Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Ndugu mmoja na mke wake waliishi Mbarara, mji mdogo ulio katika sehemu yenye milima-milima upande wa kusini magharibi, kilomita 300 hivi kutoka Kampala. Walikuwa wakifanya Funzo la Mnara wa Mlinzi na funzo la kitabu katika nyumba yao. Hata hivyo, mara kwa mara walifunga safari ndefu ya kwenda Kampala au Entebbe ili kufurahia ushirika wa Kikristo. Pia waliendelea kuwasiliana na ofisi ya tawi ya Luanshya, Rhodesia ya Kaskazini (ambako leo ni Zambia), iliyokuwa ikisimamia kazi ya kuhubiri Ufalme katika eneo la Afrika Mashariki.

  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Katika miaka ya 1970, tulifurahia kuhubiri na kushirikiana na wamishonari waliokuwa wakiishi Mbarara, kilomita 65 hivi kutoka kwetu. Siku moja, tulipokuwa tukienda kuwatembelea, wanajeshi walitusimamisha. Mmoja wao akatuambia: “Ikiwa mnataka kufa, endeleeni na safari yenu.” Tukaamua kurudi. Baada ya siku kadhaa, tukaanza kuwa na wasiwasi kuhusu wamishonari hao. Tulitaka sana kufika wanakoishi ili kuwajulia hali. Kulikuwa na ulinzi mkali sana. Nililazimika kutumia cheo changu katika hospitali na kibandiko cha hospitali kwenye gari kupita vizuizi vya barabarani. Tulifurahi sana kuwapata wamishonari hao wakiwa salama. Tuliwanunulia vyakula na kukaa nao siku kadhaa. Kisha tukawa tukiwatembelea kila juma mpaka kulipokuwa na usalama wa kutosha kuhamia Kampala.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki