-
Uganda2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Baadaye, serikali ya kikoloni ilipomwamuru Ndugu na Dada Smith waondoke Tanganyika, walifunga safari hadi Kampala, Uganda. Hata hivyo wakati huo hali haikuwa nzuri, nao polisi mjini Kampala walikuwa wakifuatia nyendo zao. Licha ya hayo, kwa muda wa miezi miwili tu, Ndugu na Dada Smith waligawa vitabu na vijitabu 2,122 na kufanya mikutano ya watu wote mara sita.
-
-
Uganda2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mwaka huohuo, Eric Cooke, kutoka ofisi ya tawi ya Rhodesia ya Kusini (ambako leo ni Zimbabwe), alizuru Afrika Mashariki na kushirikiana kwa muda na kutaniko hilo jipya mjini Kampala. Ijapokuwa akina ndugu walikuwa na mkutano wa funzo la Mnara wa Mlinzi kila juma, hawakuwa wa kawaida sana katika huduma ya Kikristo. Hivyo, Ndugu Cooke alimtia moyo Ndugu Kilminster wawe na mikutano yote ya kutaniko, kutia ndani Mkutano wa Utumishi kila juma.
-