Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Siku moja mwaka wa 70 na kitu, Peter Gyabi alikuwa akihubiri pamoja na Fred Nyende, aliyekuwa tineja wakati huo. Fred alikuwa mchanga mama yake alipojifunza kweli mwaka wa 1962. Hata hivyo, alikuwa amekua, nayo hali iliyozuka ilipima ukomavu wake.

      Mwenye nyumba mkali—ambaye yaonekana alikuwa askari kanzu—aliwatambua ndugu hao kuwa Mashahidi wa Yehova. Aliwakamata na kuwalazimisha kuingia katika gari lake. Hawakujua litakalotokea kwa sababu kwa kawaida maelfu ya watu waliokamatwa hivyo hawakuonekana tena. Pia, ilikuwa kawaida kwa watu kuteswa, iwe kuna sababu au la. Wakiwa njiani kuelekea kwenye kituo cha polisi, Peter na Fred walimwomba Yehova awape nguvu za kuwa watulivu na kudumisha uaminifu. Mtu huyo aliwapeleka kwa ofisa mkuu, akiwashtaki na kuwauliza maswali yasiyo na mwisho. Hata hivyo, Peter na Fred walijionea wenyewe ukweli wa maneno ya Methali 25:15: “Kwa subira kiongozi hushawishiwa, na ulimi wa upole unaweza kuvunja mfupa.” Hata hivyo, hakuna mfupa wowote uliovunjwa alasiri hiyo. Kwa kuwa Peter aliwaeleza kwa utulivu kuhusu msimamo wetu wa kutii sheria na kushikamana kwetu na mafundisho ya Biblia, na pia kwa kuwa ndugu hao walijiendesha na kujibu kwa heshima, hatimaye chuki ya mkuu huyo ilianza kupungua. Matokeo?

      Mkuu huyo alimwachilia Peter na Fred na kumwamuru mtu huyo aliyewakamata awarudishe katika eneo! “Dereva” wao aliyekuwa amedhalilishwa akakubali shingo-upande, nao ndugu hao wakamshukuru Yehova kwa kuwaokoa.

  • Uganda
    2010 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Picha katika ukurasa wa 95]

      Fred Nyende

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki