Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Ni Bwana”
    Mkaribie Yehova
    • Fikiria itikio la Isaya aliposikia maserafi wakitangaza utakatifu wa Yehova. “Ndipo niliposema, Ole wangu! kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi.” (Isaya 6:5) Ndiyo, utakatifu wa Yehova usio na kikomo ulimkumbusha Isaya kwamba yeye ni mwenye dhambi na mtu asiyekamilika. Mwanzoni, mwanamume huyo mwaminifu alifadhaika sana. Lakini Yehova hakumwacha akiwa katika hali hiyo.

      18 Serafi alimfariji nabii huyo mara moja. Jinsi gani? Kiumbe huyo wa roho mwenye nguvu alipaa kwenye madhabahu, akatwaa kaa la moto, akagusa kinywa cha Isaya kwa kaa hilo. Huenda hilo likaonekana kuwa jambo lenye kuumiza sana badala ya kufariji. Hata hivyo, kumbuka kwamba hilo lilikuwa ono lenye maana nyingi ya mfano. Isaya, Myahudi mwaminifu, alijua vyema kwamba dhabihu zilitolewa kila siku kwenye madhabahu ya hekalu ili kulipia dhambi. Na kwa upendo, serafi huyo alimkumbusha nabii huyo kwamba ijapokuwa alikuwa “mtu mwenye midomo michafu” asiyekamilika, bado angeweza kuwa mwadilifu machoni pa Mungu.a Yehova alikuwa tayari kumwona mwanadamu asiyekamilika, na mwenye dhambi kuwa mtakatifu—angalau kwa kadiri fulani.—Isaya 6:6, 7.

  • “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, Ni Bwana”
    Mkaribie Yehova
    • a Maneno “mwenye midomo michafu” yanafaa, kwa kuwa midomo mara nyingi hutumiwa kitamathali katika Biblia kurejezea usemi au lugha. Sehemu kubwa ya dhambi za wanadamu wote wasiokamilika, yamkini zinahusiana na jinsi tunavyotumia uwezo wetu wa kusema.—Mithali 10:19; Yakobo 3:2, 6.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki