-
Shark Bay—Eneo la Ajabu la BahariniAmkeni!—2007 | Julai
-
-
Shark Bay—Eneo la Ajabu la Baharini
NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI AUSTRALIA
SHARK BAY (Ghuba ya Papa) ni ghuba kubwa iliyo kwenye sehemu ya mashariki zaidi ya Australia, kilomita 650 kaskazini mwa jiji la Perth. Mnamo 1629, mvumbuzi Mholanzi Francois Pelsaert alisema kwamba eneo hilo la jangwa ni “nchi kavu iliyolaaniwa, ambako hakuna nyasi zozote zinazoweza kuota.” Wageni walipaita Mahali Pasipo na Matumaini, Mahali Pasipofaa Kitu, na Mahali Penye Kuvunja Moyo.
Hata hivyo, leo zaidi ya watu 120,000 hutembelea eneo hilo kila mwaka. Eneo hilo linavutia sana hivi kwamba liliingizwa kwenye Orodha ya Maeneo Yanayostahili Kuhifadhiwa Ulimwenguni mwaka wa 1991.a
-
-
Shark Bay—Eneo la Ajabu la BahariniAmkeni!—2007 | Julai
-
-
a Maeneo yenye thamani ya kipekee ya kitamaduni au kiasili hutiwa kwenye Orodha ya Maeneo Yanayostahili Kuhifadhiwa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi, na Utamaduni.
-