Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kujiua Tatizo Lililojificha Linaloenea Kasi
    Amkeni!—2000 | Februari 22
    • Mnamo mwaka wa 1996 Vituo vya Kudhibiti Magonjwa vya Marekani viliripoti kwamba idadi ya visa vya kujiua miongoni mwa Wamarekani wenye umri wa miaka 65 na zaidi iliongezeka ghafula kwa asilimia 36 tangu mwaka wa 1980. Idadi kubwa ya Wamarekani wazee-wazee walichangia ongezeko hilo—japo si hao tu. Idadi halisi ya watu wenye umri unaozidi miaka 65 waliojiua mwaka wa 1996 iliongezeka pia, kwa asilimia 9, mara ya kwanza kwa muda wa miaka 40. Kuhusu vifo vilivyotokana na majeraha, Wamarekani wengi wazee-wazee walikufa kutokana na kuanguka na aksidenti za magari peke yake. Kwa kweli, huenda hata takwimu hizi zenye kushtua zikawa chini sana. “Yashukiwa kwamba takwimu hizo zinazotegemea hati zinazoeleza kisababishi cha kifo zinataja visa vichache sana vya kujiua,” chasema kitabu A Handbook for the Study of Suicide. Kitabu hicho chaongezea kwamba watu fulani wanakadiria takwimu halisi kuwa maradufu zaidi ya takwimu zilizoripotiwa.

      Matokeo ni nini? Marekani sawa na nchi nyinginezo nyingi, inakumbwa na tatizo lililojificha linaloenea kasi tufeni pote la kujiua kwa raia wazee-wazee. Dakt. Herbert Hendin, mtaalamu wa tatizo la kujiua, asema: “Licha ya kwamba visa vya kujiua katika Marekani huongezeka kwa kawaida kulingana na umri, kujiua miongoni mwa watu wazee-wazee hakuzingatiwi sana na umma.” Mbona iwe hivyo? Yeye adokeza kwamba sehemu ya tatizo hilo ni kwa sababu visa vya watu wazee-wazee kujiua vimekuwa vingi sikuzote, “havijazusha hofu ya ghafula kama ongezeko kubwa la vijana kujiua.”

  • Kujiua Tatizo Lililojificha Linaloenea Kasi
    Amkeni!—2000 | Februari 22
    • “Si kwamba tu kujiua kumeenea sana miongoni mwa wazee-wazee, bali tendo la kujiua ladhihirisha tofauti muhimu kati ya vijana na wazee,” asema Dakt. Hendin, katika kitabu chake Suicide in America. “Hasa uwiano wa majaribio halisi ya kujiua hubadilika sana miongoni mwa wazee-wazee. Miongoni mwa watu wote kwa ujumla, uwiano wa majaribio ya kujiua na kujiua halisi umekadiriwa kuwa 10 kwa 1; miongoni mwa vijana (wenye umri wa miaka 15 hadi 24), umekadiriwa kuwa 100 kwa 1; na miongoni mwa wale wenye umri unaozidi miaka 55, umekadiriwa kuwa 1 kwa 1.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki