Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Faida za Kutembelea Majumba ya Ukumbusho
    Amkeni!—2005 | Machi 8
    • Vitu vya Sanaa vya Karne Mbalimbali

      Hebu twende kwenye Jumba la Kitaifa la Maonyesho ya Sanaa. Jumba hilo lilifunguliwa mwaka wa 1941. Humo utaona vitu vya sanaa vya karne nane. Ikiwa unapenda sanaa, itafaa uanze matembezi asubuhi kwani itakuchukua saa kadhaa kutembea, kutazama, na kufikiria vitu hivyo vya kustaajabisha ikitegemea unapenda sanaa ya kipindi gani. Kwa kuwa kuna viti vingi, unaweza kuketi ili kuchunguza vitu hivyo au kupumzika.

      Kwa kuwa Kanisa Katoliki hasa ndilo lililodhamini vitu vingi vya sanaa vya karne ya 13 hadi ya 15, michoro mingi ni ya kidini. Utaona mchoro wa Giotto unaoitwa “Madonna na Mtoto,” mchoro wa Raphael unaoitwa “The Alba Madonna” (1508), na michoro ya Leonardo da Vinci. Kazi za sanaa za karne ya 16 zinatia ndani zile za Tintoretto, Titian, na wengineo. Wanafunzi wa Biblia wanaweza kufurahia mchoro wa Tintoretto “Kristo Kwenye Bahari ya Galilaya” (karibu mwaka wa 1575/1580), unaoonyesha wanafunzi wa Kristo wakiwa ndani ya mashua ya kuvua samaki inayopigwa na dhoruba. Mchoro mwingine unaohusiana na Biblia ni ule wa El Greco unaoitwa “Kristo Akisafisha Hekalu.” Linganisha njia tofauti-tofauti za uchoraji za wasanii hao. Hebu tazama mchoro wa El Greco ulio na rangi nyingi unaoonyesha utendaji mbalimbali.

      Vitu vya sanaa vya karne ya 17 vinatia ndani vile vya Rubens, Rembrandt, na wasanii wengine. Wanafunzi wa Biblia watavutiwa na Mchoro wa Rubens unaoitwa “Danieli Katika Tundu la Simba,” uliochorwa wapata mwaka wa 1615. Mwone Danieli akiwa mtulivu huku akimshukuru Mungu kwa kuokoa uhai wake. Sasa hebu tuchunguze vitu vilivyotengenezwa na wasanii Wafaransa katika karne ya 19.

      Jumba la Kitaifa la Maonyesho ya Sanaa lina baadhi ya michoro bora zaidi ya wasanii Wafaransa mbali na ile inayopatikana huko Paris. Ikiwa umeona tu michoro iliyotokezwa kwa kuiga sanaa za awali, utasisimuka sana kuona michoro ya awali ya wasanii mbalimbali. Utavutiwa sana na ustadi wa wasanii maarufu kama vile Cézanne, Manet, Renoir, Degas, na Monet. Pia kuna michoro ya pekee ya wasanii wa Marekani kama ile ya Mary Cassatt (“Watoto Wakicheza Ufuoni”), James Abbott McNeill Whistler (“Msichana Mweupe”), na Winslow Homer (“Kubebwa na Upepo”).

      Huenda ungependa kutembelea jumba la maonyesho liitwalo East Building, ambalo lina vitu vya sanaa ya kisasa. Kuna michongo mikubwa ndani ya ua wa jengo hilo ambayo ilichongwa na Alexander Calder, Henry Moore, na wasanii wengine. Pia utaona kitambaa kilichofumwa na msanii wa Catalonia anayeitwa Joan Miró.

      Ni wazi kwamba itakuchukua muda mrefu kutembelea sehemu zote za jumba hilo la maonyesho.

  • Faida za Kutembelea Majumba ya Ukumbusho
    Amkeni!—2005 | Machi 8
    • [Picha katika ukurasa wa 18]

      Mchoro wa Winslow Homer unaoitwa “Kubebwa na Upepo,” unaopatikana katika Jumba la Kitaifa la Maonyesho ya Sanaa

      [Hisani]

      Winslow Homer, Breezing Up (A Fair Wind), Gift of the W. L. and May T. Mellon Foundation, Image © Board of Trustees, National Gallery of Art, Washington

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki