Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Waliokoka kwa Kutii Maonyo
    Amkeni!—2006 | Juni
    • Kuwatafuta Mashahidi Ndani ya Ukumbi wa Michezo

      Wakimbizi wapatao 16,000, wengi wao kutoka Louisiana, walikuwa wakipewa chakula, maji, na makao katika ukumbi wa michezo wa Astrodome huko Houston, Texas. Halmashauri ya Mashahidi ya kutoa misaada huko Houston ilipata habari kwamba kulikuwa na Mashahidi kadhaa kati ya umati huo mkubwa. Lakini wangewatafutaje?

      Mapema asubuhi ya Ijumaa, Septemba 2, kikundi cha wazee Wakristo walienda kuwatafuta akina ndugu kwenye ukumbi huo. Walishangaa kuwaona maelfu ya wanaume, wanawake, matineja, watoto na vitoto waliokuwa wamejaa katika ukumbi huo mkubwa. Uwanja huo wa mpira ulikuwa umejaa maelfu ya vitanda vidogo. Nao wakimbizi walikuwa wakisubiri kutatuliwa matatizo yao. Watu wengi walikuwa wamepanga mistari mirefu ili kupokea matibabu nao wafanyakazi wa kitiba walikuwa wakikimbia kuwapeleka wagonjwa kwenye ambulansi.

      “Nilihisi kana kwamba nilikuwa katikati ya kambi ya wakimbizi,” akasema Samuel, mmoja wa wazee aliyekuwa akiwatafuta Mashahidi wenzake. Wangewapataje Mashahidi wachache kati ya umati huo mkubwa? Wazee hao walianza kuwatafuta kwa kutembea kwenye vijia wakiwa na mabango makubwa ya kuwaomba Mashahidi wajitambulishe. Baada ya kufanya hivyo kwa muda wa saa tatu bila mafanikio walitambua kwamba walihitaji kutumia mbinu nyingine inayofaa zaidi. Waliwaomba wafanyakazi wa shirika la Msalaba Mwekundu watangaze hivi kwa kutumia vikuza-sauti: “Mashahidi wote wa Yehova waliobatizwa, tafadhali nendeni kwenye jukwaa lililo upande wa chini wa mashariki mwa ukumbi.”

      Hatimaye, Mashahidi walianza kumiminika mahali hapo huku wakitabasamu. Samuel anasema: “Walikuwa wakitokwa na machozi ya furaha. Walitukumbatia kwa nguvu na kutushika mikono. Hawakutaka kutuachilia kwa kuogopa wasipotee katikati ya umati.” Ijumaa na Jumamosi, Mashahidi 24 walipatikana na kupelekwa kwenye kituo cha kutoa misaada cha Mashahidi.

      Wengi wao walikuwa wamepoteza kila kitu isipokuwa tu mavazi machafu waliyokuwa wamevaa. Shahidi mmoja alikuwa amebeba sanduku dogo lililotoshana na katoni ya viatu. Lilikuwa na hati muhimu ambazo ndizo tu aliweza kuokoa dhoruba hiyo kali ilipotokea.

      Katika ukumbi huo, watu wengi walitambua kwamba wazee hao waliokuwa wamewatembelea ni Mashahidi wa Yehova nao waliwakaribia na kuwaomba Biblia na vichapo vya Biblia. Waliomba Biblia zaidi ya 220. Mashahidi hao pia waliwapa watu toleo la Amkeni! la Julai 22, 2005, lililokuwa na makala zilizofaa wakati huo zenye kichwa “Je, Misiba ya Asili Inaongezeka?”

  • Waliokoka kwa Kutii Maonyo
    Amkeni!—2006 | Juni
    • [Picha katika ukurasa wa 16, 17]

      Ukumbi wa Astrodome huko Houston, Texas, ulitumiwa na watu 16,000 hivi

      [Picha katika ukurasa wa 17]

      Wazee Wakristo waliwatafuta Mashahidi kati ya watu waliohamishwa

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki