Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Kuimarisha Uhakikisho wa Uhuru

      Mojawapo ya kesi za kwanza zinazohusiana na huduma ya Mashahidi wa Yehova kufikia Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani ilitoka katika Georgia na ilijadiliwa mbele ya Mahakama hiyo mnamo Februari 4, 1938. Alma Lovell alikuwa ameshtakiwa katika mahakama ya Griffin, Georgia, juu ya kukiuka sheria iliyokataza kugawanywa kwa fasihi za aina yoyote bila kibali cha mkuu wa jiji. Miongoni mwa mambo mengine, Dada Lovell alikuwa amewatolea watu gazeti The Golden Age. Mnamo Machi 28, 1938, Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani iliamua kwamba sheria hiyo haikufaa kwa sababu ilizuia uhuru wa uandishi na kuleta ukaguzi.c

      Mwaka uliofuata J. F. Rutherford, akiwa wakili wa mlalamishi, alitoa hoja katika Mahakama Kuu Zaidi katika kesi ya Clara Schneider v. State of New Jersey.d Hiyo ilifuatwa, katika 1940 na Cantwell v. State of Connecticut,e ambayo J. F. Rutherford aliandika hoja za kisheria naye Hayden Covington akatoa hoja kwa maneno mbele ya Mahakama. Matokeo yenye kufaa ya kesi hizo yaliegemeza uhakikisho wa kikatiba wa uhuru wa dini, uhuru wa usemi, na uhuru wa uandishi.

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Wakati wa miaka mitatu iliyofuata, Mahakama Kuu Zaidi iliamua dhidi ya Mashahidi wa Yehova katika kesi 19. Wenye kutokeza zaidi ulikuwa ni uamuzi usiopendeleka, wa mwaka 1942, katika kesi ya Jones v. City of Opelika.l Rosco Jones alikuwa ameshtakiwa kwa kushiriki katika kugawanya fasihi katika barabara za jiji la Opelika, Alabama, bila kulipa kodi ya leseni. Mahakama Kuu Zaidi iliunga mkono hukumu hiyo na kusema kwamba serikali zina haki ya kutoza kiasi kinachofaa cha ada kwa ajili ya kuombaomba na kwamba sheria kama hizo hazingeweza kupingwa hata ikiwa wenye mamlaka wenyeji huenda wakabatilisha ile leseni. Hilo lilikuwa pigo kubwa, kwa sababu sasa jumuiya yoyote, ikichochewa na makasisi au mtu mwingine yeyote aliyepinga Mashahidi, ingeweza kuwapuuza kisheria na hivyo wapinzani huenda wakawaza kwamba hilo lingekomesha utendaji wa kuhubiri wa Mashahidi wa Yehova. Lakini jambo lisilo la kawaida likatukia.

      Hali Yabadilika

      Katika kesi ya Jones v. Opelika, ule uamuzi ambao ulikuwa pigo kubwa kwa huduma ya hadharani ya Mashahidi wa Yehova, mahakimu watatu kati ya wengine walisema kwamba, wao hawakukubaliana na uamuzi wa walio wengi Mahakamani juu ya kesi hiyo na pia walihisi kwamba walikuwa wamesaidia kuweka msingi wayo katika kesi ya Gobitis. “Kwa kuwa tuliungana katika maoni katika kesi ya Gobitis,” wakaongeza, “tunafikiri hii ni pindi inayofaa kusema kwamba sasa tunaamini kwamba hiyo pia iliamuliwa vibaya.” Mashahidi wa Yehova waliona hiyo kuwa ishara ya kupeleka masuala hayo upya Mahakamani.

      Maombi ya Kusikizwa Tena kwa kesi yalipelekwa katika kesi ya Jones v. Opelika. Katika maombi hayo, hoja za kisheria zenye nguvu zilitolewa. Pia yalijulisha hivi kwa imara: “Mahakama hii yapasa ifahamu jambo kuu la hakika, kwamba inashughulika kisheria na watumishi wa Mungu Mweza Yote.” Mifano ya Kibiblia iliyotangulia ikionyesha maana ya hayo ilipitiwa. Uangalifu ulielekezwa kwenye shauri lililotolewa na mwalimu wa torati Gamalieli kwa mahakama kuu ya Kiyahudi ya karne ya kwanza, yaani: “Msijiingize katika mambo ya watu hawa, bali waacheni; . . . ama sivyo, huenda [labda] mkaonwa kuwa wapiganaji dhidi ya Mungu kwa kweli.”—Mdo. 5:34-39, NW.

      Hatimaye, katika Mei 3, 1943, katika kesi ya maana sana ya Murdock v. Commonwealth of Pennsylvania,a Mahakama Kuu Zaidi ilibatilisha uamuzi wayo wa kwanza katika kesi ya Jones v. Opelika. Ilijulisha kwamba kodi yoyote ya leseni inayoitishwa kwanza ili mtu aweze kuwa na uhuru wa dini wa kugawanya fasihi za kidini ni jambo lisilo la kikatiba. Kesi hiyo iliandaa fursa kwa Mashahidi wa Yehova katika Marekani na imerejezewa kuwa kiolezo katika mamia ya kesi tangu wakati huo. Mei 3, 1943, ilikuwa siku ya kukumbukwa kikweli kwa Mashahidi wa Yehova kuhusiana na mashtaka mbele ya Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani. Katika siku hiyo moja, kesi 12 kati ya 13 (zote zikiwa zimejumlishwa ziweze kusikizwa na kuamuliwa katika maamuzi manne), Mahakama iliamua kwa kuwapendelea.b

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Sanduku katika ukurasa wa 688]

      “Aina ya Uenezaji-Evanjeli wa Wamishonari Ulio wa Kikale”

      Katika 1943, katika kesi ya “Murdock v. Pennsylvania,” Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani ilisema hivi, miongoni mwa mambo mengine:

      “Kugawanywa kwa trakti za kidini kwa mkono ni aina ya uenezaji-evanjeli wa wamishonari ulio wa kikale—wa kale kama historia ya matbaa ya uchapaji. Kumekuwa kani yenye nguvu katika mashirika mbalimbali ya kidini kwa muda wa miaka mingi. Aina hiyo ya uenezaji-evanjeli inatumiwa leo kwa kiwango kikubwa na mafarakano mbalimbali ya kidini ambayo makolpota wayo hupeleka Gospeli kwa maelfu na maelfu ya makao na hutafuta kupata wenye kushikamana na imani yao kupitia ziara za kibinafsi. Ni zaidi ya kuhubiri; ni zaidi ya kugawanya fasihi za kidini. Ni jumla ya hayo yote mawili. Kusudi layo ni kueneza evanjeli kama lile la mkutano wa kuhuisha. Aina hiyo ya utendaji wa kidini ni ya cheo kilekile cha juu chini ya Rekebisho la Kwanza kama vile ibada katika makanisa na mahubiri kutoka kwa mimbari. Hudai ulinzi uleule ambao utendaji mwingineo wa kidini unaokubalika na ulio wa kawaida hupewa. Pia hudai uhakikisho wa uhuru wa usemi na uhuru wa uandishi kama ule mwingineo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki