Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Hali Yabadilika

      Katika kesi ya Jones v. Opelika, ule uamuzi ambao ulikuwa pigo kubwa kwa huduma ya hadharani ya Mashahidi wa Yehova, mahakimu watatu kati ya wengine walisema kwamba, wao hawakukubaliana na uamuzi wa walio wengi Mahakamani juu ya kesi hiyo na pia walihisi kwamba walikuwa wamesaidia kuweka msingi wayo katika kesi ya Gobitis. “Kwa kuwa tuliungana katika maoni katika kesi ya Gobitis,” wakaongeza, “tunafikiri hii ni pindi inayofaa kusema kwamba sasa tunaamini kwamba hiyo pia iliamuliwa vibaya.” Mashahidi wa Yehova waliona hiyo kuwa ishara ya kupeleka masuala hayo upya Mahakamani.

      Maombi ya Kusikizwa Tena kwa kesi yalipelekwa katika kesi ya Jones v. Opelika. Katika maombi hayo, hoja za kisheria zenye nguvu zilitolewa. Pia yalijulisha hivi kwa imara: “Mahakama hii yapasa ifahamu jambo kuu la hakika, kwamba inashughulika kisheria na watumishi wa Mungu Mweza Yote.” Mifano ya Kibiblia iliyotangulia ikionyesha maana ya hayo ilipitiwa. Uangalifu ulielekezwa kwenye shauri lililotolewa na mwalimu wa torati Gamalieli kwa mahakama kuu ya Kiyahudi ya karne ya kwanza, yaani: “Msijiingize katika mambo ya watu hawa, bali waacheni; . . . ama sivyo, huenda [labda] mkaonwa kuwa wapiganaji dhidi ya Mungu kwa kweli.”—Mdo. 5:34-39, NW.

      Hatimaye, katika Mei 3, 1943, katika kesi ya maana sana ya Murdock v. Commonwealth of Pennsylvania,a Mahakama Kuu Zaidi ilibatilisha uamuzi wayo wa kwanza katika kesi ya Jones v. Opelika. Ilijulisha kwamba kodi yoyote ya leseni inayoitishwa kwanza ili mtu aweze kuwa na uhuru wa dini wa kugawanya fasihi za kidini ni jambo lisilo la kikatiba. Kesi hiyo iliandaa fursa kwa Mashahidi wa Yehova katika Marekani na imerejezewa kuwa kiolezo katika mamia ya kesi tangu wakati huo. Mei 3, 1943, ilikuwa siku ya kukumbukwa kikweli kwa Mashahidi wa Yehova kuhusiana na mashtaka mbele ya Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani. Katika siku hiyo moja, kesi 12 kati ya 13 (zote zikiwa zimejumlishwa ziweze kusikizwa na kuamuliwa katika maamuzi manne), Mahakama iliamua kwa kuwapendelea.b

      Karibu mwezi mmoja baadaye—mnamo Juni 14, Siku ya Bendera ya kila mwaka ya taifa—Mahakama Kuu Zaidi tena ilibadili uamuzi wayo, wakati huu kuhusiana na uamuzi katika kesi ya Gobitis, wakifanya hivyo katika kesi iliyoitwa West Virginia State Board of Education v. Barnette.c Iliamua kwamba “hakuna ofisa, wa juu au wa chini, awezaye kuonyesha yale yanayokubalika na ya kweli katika siasa, utukuzo wa taifa, dini, au mambo mengineyo au kuwalazimisha raia waungame kwa maneno au watende kupatana na imani yao.” Hoja nyingi zilizotolewa katika uamuzi huo zilitumiwa baadaye nchini Kanada na Mahakama ya Rufani ya Ontario katika kesi ya Donald v. Hamilton Board of Education, na Mahakama Kuu Zaidi ya Kanada ilikataa kubatilisha uamuzi huo.

      Kupatana na uamuzi wayo katika kesi ya Barnette, na katika siku hiyohiyo, katika kesi ya Taylor v. State of Mississippi,d Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani iliamua kwamba Mashahidi wa Yehova hawangeweza kwa kufaa kushtakiwa uhaini kwa kueleza sababu zao za kutosalimu bendera na kwa kufundisha kwamba mataifa yote yako upande wa ushinde kwa sababu yanapinga Ufalme wa Mungu. Maamuzi hayo pia yalitayarisha njia kwa maamuzi yaliyofuata yenye kupendeleka katika mahakama nyinginezo katika kesi zilizohusu wazazi Mashahidi ambao watoto wao walikuwa wamekataa kusalimu bendera shuleni, pamoja na katika masuala yaliyohusu uajiri na utunzi wa watoto. Hali ilikuwa imebadilika kabisa.e

  • “Kutetea na Kuthibitisha Kisheria Habari Njema”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Sanduku katika ukurasa wa 687]

      Matukio Yaliyotangulia Kubadilishwa kwa Uamuzi

      Katika 1940, wakati Mahakama Kuu Zaidi ya Amerika ilipoamua, katika kesi ya “Minersville School District v. Gobitis,” kwamba watoto wa shule wangetakiwa kusalimu bendera, mahakimu wanane kati ya tisa waliunga mkono uamuzi huo. Ni Hakimu Stone pekee aliyepinga. Lakini miaka miwili baadaye, walipokuwa wakiandikisha tofauti zao katika kesi ya “Jones v. Opelika,” mahakimu wengine watatu (Black, Douglas, na Murphy) walitumia pindi hiyo kusema kwamba waliamini kwamba kesi ya “Gobitis” ilikuwa imeamuliwa vibaya kwa sababu ilikuwa imeshusha uhuru wa kidini. Hiyo ilimaanisha kwamba mahakimu wanne kati ya tisa waliunga mkono kubadilishwa kwa uamuzi katika kesi ya “Gobitis.” Mawakili wawili kati ya wale watano waliokuwa wamepuuza uhuru wa kidini walistaafu. Kulikuwa na wengine wawili wapya (Rutledge na Jackson) wakati kesi iliyofuata ya kusalimu bendera ilipopelekwa kwenye Mahakama Kuu Zaidi. Katika 1943, katika kesi ya “West Virginia State Board of Education v. Barnette,” wote wawili waliunga mkono uhuru wa kidini badala ya jambo la kushurutishwa kusalimu bendera. Hivyo, huku mahakimu 6 dhidi ya 3 zikiunga mkono, mahakama ilibadilisha msimamo iliyokuwa imechukua katika kesi tano za mapema (“Gobitis,” “Leoles,” “Hering,” “Gabrielli,” na “Johnson”) zilizokuwa zimekatwa rufani katika Mahakama hiyo.

      Kwa kupendeza, katika kupinga uamuzi wa kesi ya “Barnette,” Hakimu Frankfurter alisema hivi: “Kama vile imekuwa katika nyakati zilizopita, Mahakama itabadilisha msimamo wayo mara kwa mara. Lakini ninaamini kwamba Mahakama hii haijapata kamwe kubatilisha maamuzi yayo ili kupunguza uwezo wa serikali ya kidemokrasia, kabla ya kesi hizi za Mashahidi wa Yehova (isipokuwa mabadiliko madogomadogo yaliyopatikana baadaye).”

      [Sanduku katika ukurasa wa 688]

      “Aina ya Uenezaji-Evanjeli wa Wamishonari Ulio wa Kikale”

      Katika 1943, katika kesi ya “Murdock v. Pennsylvania,” Mahakama Kuu Zaidi ya Marekani ilisema hivi, miongoni mwa mambo mengine:

      “Kugawanywa kwa trakti za kidini kwa mkono ni aina ya uenezaji-evanjeli wa wamishonari ulio wa kikale—wa kale kama historia ya matbaa ya uchapaji. Kumekuwa kani yenye nguvu katika mashirika mbalimbali ya kidini kwa muda wa miaka mingi. Aina hiyo ya uenezaji-evanjeli inatumiwa leo kwa kiwango kikubwa na mafarakano mbalimbali ya kidini ambayo makolpota wayo hupeleka Gospeli kwa maelfu na maelfu ya makao na hutafuta kupata wenye kushikamana na imani yao kupitia ziara za kibinafsi. Ni zaidi ya kuhubiri; ni zaidi ya kugawanya fasihi za kidini. Ni jumla ya hayo yote mawili. Kusudi layo ni kueneza evanjeli kama lile la mkutano wa kuhuisha. Aina hiyo ya utendaji wa kidini ni ya cheo kilekile cha juu chini ya Rekebisho la Kwanza kama vile ibada katika makanisa na mahubiri kutoka kwa mimbari. Hudai ulinzi uleule ambao utendaji mwingineo wa kidini unaokubalika na ulio wa kawaida hupewa. Pia hudai uhakikisho wa uhuru wa usemi na uhuru wa uandishi kama ule mwingineo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki