Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 21. (a) Wale maadui wa kidini wa mashahidi wawili walitumiaje kwa faida yao hali ya vita? (b) Uhakika wa kwamba zile maiti za mashahidi wawili ziliachwa bila kuzikwa ulionyesha nini? (c) Kipindi cha wakati cha siku tatu na nusu chapasa kionweje? (Ona kielezi cha chini.)

      21 Kutoka 1914 kufika 1918 mataifa yalikuwa yakishughulika na vita ya kwanza ya ulimwengu. Hisi za utukuzaji wa taifa zilipanda juu, na katika masika ya 1918, maadui wa kidini wa mashahidi wawili walijifaidi na hali hiyo. Walitumia kwa hila chombo cha Serikali cha kisheria hivi kwamba wahudumu wenye madaraka miongoni mwa Wanafunzi wa Biblia walitiwa gerezani kwa mashtaka bandia ya kufitini serikali. Wafanya kazi wenzi waaminifu waliduwaa.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika kitabu chake Preachers Present Arms, kilichotangazwa katika 1933, Ray H. Abrams anarejezea upinzani mkali wa viongozi wa kidini kuelekea kitabu cha Wanafunzi wa Biblia The Finished Mystery. Yeye hupitia jitihada za viongozi wa kidini za kuondolea mbali Wanafunzi wa Biblia na “usadikishi [wao] wenye kusumbua sana.” Hiyo iliongoza kwenye kesi ya mahakamani iliyokuwa na tokeo la kuhukumia J. F. Rutherford na waandamani wenzake saba miaka mirefu gerezani. Dakt. Abrams anaongezea: “Uchanganuzi wa kesi yote hiyo unaongoza kwenye mkataa wa kwamba makanisa na viongozi wa kidini mwanzoni ndio walioanza mwendo wa kufutilia mbali Waruseli.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Dakt. Abrams anaendelea: “Wakati habari za hukumu ya vifungo hivyo vya miaka ishirini zilipowafikia wahariri wa magazeti ya kidini, karibu kila kimoja cha vichapo hivyo, kikubwa na kidogo, kilishangilia tukio hilo. Mimi nimeshindwa kuona maneno yoyote ya kusikitikia katika lolote la majarida hayo ya dini zilizokubaliwa. ‘Hakuwezi kuwa na shaka,’ akakata maneno Upton Sinclair, kwamba ‘mnyanyaso . . . ulianza kwa sehemu kutokana na uhakika wa kwamba wao walikuwa wamejiletea chuki ya vikundi vya kidini “vilivyokubaliwa.”’ Kile ambacho jitihada za pamoja za makanisa zilikuwa zimeshindwa kufanya sasa inaonekana serikali ilikuwa imefaulu kuwatimizia.” Baada ya kunukuu maelezo yenye kuvunja heshima ya vichapo kadhaa vya kidini, mwandikaji huyo alirejezea badiliko la uamuzi katika Mahakama ya Rufani akaeleza: “Uamuzi huu ulipokewa na makanisa kwa ukimya.”

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 24. Mashahidi wawili walipokuja kwenye uhai tokeo lilikuwa nini kwa wanyanyasi wao wa kidini?

      24 Ulikuwa mshtuko kama nini kwa wanyanyasi hao! Ghafula maiti za mashahidi wawili zikawa hai tena na zenye kutenda. Viongozi wa kidini hao waliona uchungu sana, na zaidi hivyo kwa kuwa wahudumu hao Wakristo ambao walikuwa wametungia hila wawaweke katika gereza walikuwa huru tena, na baadaye wakaondolewa mashtaka kabisa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki