-
Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Matbaa ya kwanza kati ya zile tatu huko Wallkill ilipelekwa kwenye jengo jipya mwezi wa Desemba. Matbaa mpya mbili zililetwa Aprili na Mei 2004 na kuanza kufanya kazi Juni na Julai. Mnamo Septemba matbaa zote tano zilikuwa zinafanya kazi.
-
-
Matukio Muhimu Ya Mwaka Uliopita2005 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Mabadiliko Huko Brooklyn
Mambo yamebadilika katika Betheli ya Brooklyn baada ya kuhamishwa kwa idara ya uchapaji, ujalidi, na usafirishaji. Aprili 29, 2004 ilikuwa pindi muhimu na yenye kugusa hisia. Jioni hiyo, ndugu walishangilia na kutoa machozi, wakati Max Larson, ambaye amesimamia idara ya uchapaji kwa zaidi ya miaka 60, alipofunga matbaa ya mwisho huko Brooklyn na kukomesha kazi ya uchapaji iliyokuwa imeendelea mfululizo kwa miaka 84. Idara ya ujalidi ilifungwa majuma kadhaa baadaye.
-