Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wakati wa Kutahini (1914-1918)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Si kila mtu aliyesisimuliwa na mafanikio ya The Finished Mystery. Kitabu hicho kilikuwa na marejezo fulani kwa makasisi wa Jumuiya ya Wakristo yaliyokuwa yenye kuchoma sana. Jambo hilo liliwakasirisha sana makasisi hivi kwamba walihimiza serikali ikandamize vichapo vya Wanafunzi wa Biblia. Kama tokeo la upinzani huo wenye kuchochewa na makasisi, mapema katika 1918, The Finished Mystery kilipigwa marufuku katika Kanada. Upesi upinzani ukapanda dhidi ya Wanafunzi wa Biblia katika Marekani.

      Ili kufichua wazi msongo huu wenye kuchochewa na makasisi, katika Machi 15, 1918, Watch Tower Society ilitoa trakti Kingdom News Na. 1. Ujumbe wayo ulikuwa nini? Kichwa kikuu cha makala chenye upana wa safu sita kilisomeka hivi: “Utovu wa Uvumilio wa Kidini—Wafuasi wa Pasta Russell Wanyanyaswa Kwa Sababu Wawaambia Watu Kweli.” Chini ya kichwa kikuu “Wanayotendwa Wanafunzi wa Biblia Yafanana na Yale ya ‘Enzi za Giza’” yaliandikwa mambo ya hakika ya mnyanyaso na marufuku iliyokuwa imeanza Kanada. Wachochezi ni nani? Trakti hiyo haikuficha kweli ikielekeza kwa makasisi, ambao walielezwa kuwa “jamii ya wanaume wenye kushikilia kauli yao ambao sikuzote wamejitahidi kuzuia watu wasiielewe Biblia na kukandamiza mafundisho yote ya Biblia isipokuwa kama yamekuja kupitia kwao.”e Lo, ni ujumbe wenye kupiga kwa nguvu kama nini!

      Makasisi waliitikiaje mfichuo huo? Tayari walikuwa wamechochea matata dhidi ya Watch Tower Society. Lakini sasa walitenda kikatili! Katika masika ya 1918, wimbi la mnyanyaso lilianzishwa dhidi ya Wanafunzi wa Biblia katika Amerika Kaskazini na Ulaya pia. Upinzani huo wenye kuchochewa na makasisi ulifikia upeo katika Mei 7, 1918, wakati waranti za serikali ya muungano ya Marekani zilipotolewa ili kukamata J. F. Rutherford na washirika wake kadhaa wa karibu. Kufikia katikati ya 1918, Rutherford na washirika saba walijipata wakiwa katika gereza la serikali ya muungano katika Atlanta, Georgia.

  • Wakati wa Kutahini (1914-1918)
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • [Sanduku katika ukurasa wa 70]

      Wenye Kupatwa na Mnyanyaso Uliochochewa na Makasisi

      Kufikia katikati ya 1918, J. F. Rutherford na washirika wake saba wa karibu walikuwa gerezani—wenye kupatwa na upinzani uliochochewa na makasisi. Lakini wanaume hao wanane sio peke yao waliokuwa shabaha ya chuki hiyo. Wakati wa miaka ya mapema C. T. Russell ndiye sanasana aliyekuwa shabaha ya shambulio la makasisi na magazeti ya habari. Sasa ikawa ni Wanafunzi wa Biblia ndiyo wenye kushambuliwa. “The Golden Age” (sasa “Amkeni!”) la Septemba 29, 1920, lilitangaza ripoti ndefu, yenye kueleza mambo waziwazi juu ya mnyanyaso wa kikatili waliovumilia katika Marekani. Lilisomeka kama jambo fulani kutoka katika Baraza la Kuhukumu Wazushi.g Masimulizi yafuatayo yalitiwa ndani:

      “Aprili 22, 1918, katika Wynnewood, Oklahoma, Claud Watson kwanza alitiwa katika jela kisha akaachiliwa kimakusudi mikononi mwa genge la wafanyaghasia waliokuwa makasisi, wanabiashara, na wachache wengine ambao walimwangusha chini, na kumwagiza mnegro ampige mijeledi, na alipopata nafuu kidogo, ampige mijeledi tena. Halafu wakammwagia lami na manyoya mwili wote, na kusugua lami ndani ya nywele na ngozi ya kichwa chake.”

      “Aprili 29, 1918, katika Walnut Ridge, Arkansas, W. B. Duncan, umri wa miaka 61, Edward French, Charles Franke, Bw. Griffin na Bi. D. Van Hoesen walitiwa ndani ya jela. Jela ilivunjwa na genge la wafanyaghasia ambalo lilitumia maneno ya matusi na machafu sana, likawapiga mijeledi, likawapaka lami, likawatia manyoya na kuwafukuza kutoka mjini. Duncan alishurutishwa kutembea kilometa arobaini na mbili kwenda nyumbani kwake naye hakupona kabisa. Griffin alipofushwa karibu kabisa na akafa kutokana na shambulio hilo miezi michache baadaye.”

      “Aprili 30, 1918, . . . katika Minerva, Ohio, S. H. Griffin kwanza alitiwa ndani ya jela kisha akaachiliwa mikononi mwa genge la wafanyaghasia, kisha akahutubiwa na mhudumu kwa dakika kumi na tano, kisha akapigwa tena na tena, akalaaniwa, akapigwa mateke, akakanyagwakanyagwa, akatishwa kutundikwa na kufishwa maji, akafukuzwa mjini, akatemewa mate, akakunguwazwa tena na tena, akadungwadungwa kwa mwavuli, akakatazwa asipande gari, akafuatwa kwa kilometa nane mpaka Malvern, Ohio, akakamatwa tena, akatiwa ndani ya jela kwa ajili ya ulinzi katika Carrollton na hatimaye akapelekwa nyumbani na maofisa walio wajasiri na waaminifu ambao, baada ya kuchunguza fasihi yake, walisema, kitu kama, ‘Hatuoni kosa katika mtu huyu.’”

      [Maelezo ya Chini]

      g Kur. 712-717.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki