Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Nimethawabishwa kwa Kufanya Mabadiliko
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 15
    • Chuki kuelekea jamii fulani iliongezeka hata zaidi katikati ya miaka ya 1950, na nyakati nyingine kulikuwa na jeuri. Katika mwaka wa 1954, baadhi ya Mashahidi walikasirika walipoona kwamba hakuna msemaji mweusi kwenye programu za makusanyiko kadhaa ya wilaya. Tuliwatia moyo ndugu zetu weusi wawe na subira. Kusanyiko lililofuata nikapewa mgawo wa kuwa msemaji. Baada ya hapo, ndugu zaidi weusi kutoka eneo la Kusini wakapewa migawo katika makusanyiko.

      Baada ya muda, jeuri dhidi ya jamii fulani katika eneo la Kusini ilipungua, na hatua kwa hatua makutaniko yakaanza kuungana. Hivyo wahubiri walihitaji kupangwa upya katika makutaniko mbalimbali kutia ndani kurekebisha maeneo ya makutaniko na kugawa upya majukumu ya akina ndugu waliokuwa wakisimamia. Baadhi ya ndugu fulani weupe na weusi hawakupendezwa na mpango huo mpya. Hata hivyo, ndugu na dada wengi walikuwa kama Baba yetu wa mbinguni ambaye hana ubaguzi. Kwa kweli, wengi walikuwa marafiki wakubwa licha ya rangi zao. Familia yetu ilishuhudia jambo hilo katika miaka ya 1930 na 1940 nilipokuwa nikikua.

  • Nimethawabishwa kwa Kufanya Mabadiliko
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Desemba 15
    • [Picha katika ukurasa wa 6]

      Waangalizi wanaosafiri na wake zao wakijitayarisha kwa ajili ya kusanyiko la wilaya la mchanganyiko wa watu weupe na weusi, mwaka wa 1966

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki