Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Njugu Ni Mbegu Ndogo Inayopendwa Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2003 | Aprili 22
    • Kufikia mwanzoni mwa miaka ya 1800, kilimo cha njugu kilikuwa kikiendelea huko South Carolina, Marekani. Njugu zilitumiwa kuwalisha maaskari waliokuwa wakipigana wakati wa Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe ya Marekani, ambayo ilianza mwaka wa 1861.

      Hata hivyo, watu wengi wakati huo waliona njugu kuwa chakula cha maskini. Huenda hiyo ndiyo sababu wakulima Wamarekani wa wakati huo hawakuzalisha njugu kwa wingi. Zaidi ya hayo, kabla ya mwaka wa 1900, wakati ambapo mashine za kilimo zilianza kuvumbuliwa, ilikuwa kazi ngumu sana kusitawisha njugu.

      Lakini kufikia mwaka wa 1903, Mmarekani George Washington Carver, mmojawapo wa wanakemia wa kwanza wa kilimo, alikuwa ameanza kufanya utafiti kuhusu matumizi mapya ya mmea wa njugu. Muda si muda akatengeneza zaidi ya bidhaa 300 kutokana na njugu. Bidhaa hizo zilitia ndani vinywaji, vipodozi, rangi, dawa, sabuni, dawa za kuua wadudu, na wino wa kuchapia. Carver aliwatia moyo wakulima wa nchi hiyo waache zoea la kupanda pamba tu na badala yake wapande mimea ya njugu pia katikati ya mimea ya pamba ili udongo usidhoofike. Wakati huo, mdudu fulani wa jamii ya fukusi alikuwa akiharibu mimea ya pamba, na wakulima wengi walilazimika kufuata mashauri ya Carver. Ikawaje? Mimea ya njugu ilinawiri sana hivi kwamba ikawa zao kuu kusini mwa Marekani. Hivi leo kuna mnara wa ukumbusho kwa ajili ya Carver huko Dothan, Alabama. Na mnara wa ukumbusho wa mdudu huyo mharibifu umechongwa katika mji wa Enterprise, Alabama, kwani uvamizi wake ndio uliowachochea wakulima wapande njugu.

  • Njugu Ni Mbegu Ndogo Inayopendwa Ulimwenguni Pote
    Amkeni!—2003 | Aprili 22
    • Marekani huvuna zaidi ya kilogramu bilioni moja za njugu kila mwaka. Hivyo, nchi hiyo huzalisha asilimia 10 hivi ya njugu zote zinazozalishwa ulimwenguni.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki