Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kwa Nini Ni Muhimu Kuwa na Polisi?
    Amkeni!—2002 | Julai 8
    • Hapo zamani, Stephen alikuwa afisa wa polisi huko Marekani. Anasema hivi: ‘Nilitaka kuwa polisi kwa sababu polisi ana uwezo na wakati wa kuwasaidia watu kwa njia bora zaidi wakati wanapomwomba awasaidie. Nilitaka kujitolea kuwasaidia watu. Ninahisi kwamba nilisaidia kwa kiasi fulani kuwalinda watu dhidi ya uhalifu. Niliwakamata zaidi ya watu 1,000 kwa kipindi cha miaka mitano. Lakini nilifurahi sana nilipowapata watoto waliokuwa wamepotea, nilipowasaidia wagonjwa wa akili waliokuwa wametoroka makwao, na kupata magari yaliyokuwa yameibwa. Pia, nilisisimuka nilipowafuata na kuwakamata washukiwa.’

  • Mambo Yaliyotarajiwa na Kuhofiwa Kuhusu Polisi
    Amkeni!—2002 | Julai 8
    • Mwanzo wa Jeshi la Polisi Huko Marekani

      New York City ndilo lililokuwa jiji la kwanza kuwa na jeshi la polisi huko Marekani. Kadiri jiji hilo lilivyozidi kuwa na mali, ndivyo uhalifu pia ulivyoongezeka. Kufikia miaka ya 1830, habari zenye kushtua kuhusu uhalifu zilichapwa katika magazeti yaliyouzwa kwa bei rahisi ambayo yalikuwa yameanza kuchapishwa. Watu wengi wakalalamika, na jeshi la polisi likaanzishwa huko New York mnamo mwaka wa 1845. Tangu wakati huo wakazi wa New York wamependezwa na jeshi la polisi la London na wakazi wa London wamependezwa na jeshi la polisi la New York.

      Sawa na Waingereza, Wamarekani pia waliogopa wazo la kuwa na jeshi la polisi lenye silaha ambalo lingesimamiwa na serikali. Lakini mataifa hayo mawili yalitatua jambo hilo kwa njia tofauti-tofauti. Waingereza waliamua kwamba polisi wao wangekuwa waungwana na wangevaa kofia ndefu na mavazi rasmi ya rangi ya bluu. Walibeba kirungu kifupi tu ambacho walikificha. Hadi leo hii polisi wa Uingereza hawabebi bunduki isipokuwa tu katika hali za dharura. Hata hivyo, kama vile ripoti moja inavyosema, ‘yaonekana kwamba hatimaye polisi wote wa Uingereza watalazimika kuwa na silaha.’

      Hata hivyo, watu huko Marekani waliogopa kwamba serikali ingetumia mamlaka yake vibaya na hilo lilisababisha Marekebisho ya Pili ya Katiba ya Marekani. Katiba hiyo inawapa watu ‘haki ya kuwa na silaha.’ Hivyo, polisi wakataka kuwa na bunduki. Muda si muda, wakatumia bunduki hizo walipokuwa wakiwafukuza wezi katika barabara za miji. Sababu nyingine iliyowafanya Wamarekani wawe na maoni hayo kuhusu kubeba bunduki ni kwamba jeshi la kwanza la polisi huko Marekani lilianzishwa katika hali tofauti sana na zile za London. Ghasia ziliongezeka huko New York kadiri idadi ya watu ilivyozidi kuongezeka. Baada ya Vita ya Wenyewe kwa Wenyewe iliyotokea katika mwaka wa 1861-1865, kulikuwa na ongezeko la maelfu ya wahamiaji kutoka Ulaya na vilevile Wamarekani wenye asili ya Kiafrika, na hilo lilisababisha ujeuri katika jamii. Polisi walionelea kwamba wanapaswa kuchukua hatua kali zaidi.

      Kwa hiyo, ijapokuwa polisi hawakupendwa, bado walihitajiwa. Watu walikuwa tayari kuvumilia matendo maovu ya polisi wakitumaini kwamba wangekuwa na usalama na utaratibu wa kadiri fulani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki