-
Abrahamu—Kielelezo cha ImaniMnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
Kulingana na Mwanzo 11:31, Abramu aliishi na familia yake katika mji wenye ufanisi wa “Uru wa Wakaldayo,” ambao wakati mmoja ulikuwa mashariki ya Mto Eufrati.a Hivyo, hakukua akiwa mhamaji mwenye kuishi mahemani bali alikuwa mkazi wa mji wenye anasa nyingi. Bidhaa kutoka nchi za nje zingeweza kununuliwa kwenye masoko ya Uru. Mitaa ya Uru ilikuwa na nyumba kubwa zilizopakwa chokaa ambazo zilikuwa na maji ya mfereji.
4. (a) Ni magumu gani ambayo waabudu wa Mungu wa kweli walipata huko Uru? (b) Abramu alikuja kudhihirishaje imani katika Yehova?
4 Mbali na manufaa za kimwili, maisha katika mji wa Uru yalifanya hali iwe ngumu sana kwa mtu yeyote aliyetaka kumtumikia Mungu wa kweli. Mji huo ulikolea ibada ya sanamu na ushirikina. Naam, jengo lililokuwa kubwa zaidi mjini humo ni hekalu refu lililomtukuza mungu-mwezi aitwaye Nanna.
-
-
Abrahamu—Kielelezo cha ImaniMnara wa Mlinzi—2001 | Agosti 15
-
-
a Japo sasa Mto Eufrati uko umbali wa kilometa 16 mashariki ya mahali ambapo mji wa zamani wa Uru ulikuwa, kuna uthibitisho unaoonyesha kwamba nyakati za kale mto huo ulikuwa magharibi ya mji huo. Hivyo, baadaye ingeweza kusemwa kwamba Abramu alitoka “ng’ambo ya Mto [Eufrati].”—Yoshua 24:3.
-