Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Makaburi Hutufunulia Imani za Kale
    Amkeni!—2005 | Desemba 8
    • Makaburi Hutufunulia Imani za Kale

      HEBU wazia kwamba unaishi maelfu ya miaka iliyopita. Uko katika jiji la Uru, ambalo ni jiji la kifalme lenye ufanisi huko Sumer, Babilonia. Msafara mkubwa wa Wasumeria umeondoka jijini, umefika kwenye eneo la makaburi, na sasa unateremka kuelekea kwenye kaburi la mfalme fulani aliyekufa hivi karibuni. Kuta na sakafu ya kaburi hilo zimefunikwa kwa mikeka, na chumba kimepambwa kwa vitu vya kisanaa vyenye kupendeza vya Wasumeria. Wanamuziki wanaandamana na msafara huo wa askari, watumishi, na wanawake kwenye kaburi hilo. Wote wamevalia mavazi mazuri yanayovutia. Maofisa wanafurahia kubeba nembo zinazoonyesha vyeo vyao. Kwenye msafara huo wenye kuvutia, kuna magari yanayoendeshwa na wanadamu na kukokotwa na mafahali au punda, huku watunzaji wa wanyama hao wakitembea karibu na vichwa vyao. Wote wanasimama mahali pao, na ibada ya kidini inafanywa huku muziki ukichezwa kwa ala.

      Msafara huo wa kidini unapomalizika, kila mtu, kuanzia mwanamuziki hadi mtumishi, anachukua kikombe kidogo cha udongo, mawe, au chuma alichobeba kwenye sherehe hiyo, anakichovya ndani ya chungu cha shaba, na kunywa kinywaji fulani kilichotayarishwa kwa njia maalumu. Kisha wote wanalala chini wakiwa wamejipanga kwa utaratibu, wanajistarehesha kwenye mikeka yao, wanalala usingizi, na kufa. Mtu fulani anachinja wanyama harakaharaka. Wafanyakazi waziba kijia kinachoelekea kaburini na kuliziba kaburi hilo. Wasumeria wanaamini kwamba mfalme wao aliye mungu, sasa anaelekea kwenye ulimwengu mwingine akiwa katika gari lake, pamoja na watumishi wake na askari wa kumlinda.

      Alipokuwa akifanya kazi kusini mwa Iraq, mwakiolojia, Bwana Leonard Woolley, alichimbua makaburi 16 ya wafalme katika eneo la makaburi la Uru la kale, kama lile lililotajwa. Huo ulikuwa ugunduzi wenye kutisha na usio wa kawaida. “Mali zilizo katika makaburi hayo, ambazo hazina kifani katika akiolojia ya Mesopotamia zilitia ndani baadhi ya vifaa maarufu zaidi vya kisanaa vya Wasumeria ambavyo sasa vimebandikwa kwenye kuta za Jumba la Makumbusho la Uingereza na Jumba la Makumbusho la Chuo Kikuu cha Pennsylvania,” asema Paul Bahn katika kitabu chake Tombs, Graves and Mummies.

  • Makaburi Hutufunulia Imani za Kale
    Amkeni!—2005 | Desemba 8
    • [Picha katika ukurasa wa 20]

      Vazi la kichwani na kito cha mjakazi Msumeria aliyezikwa katika kaburi la kifalme huko Uru

      [Hisani]

      © The British Museum

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki