-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2011 | Januari 1
-
-
Yaelekea Abramu (Abrahamu) aliishi katika nyumba ya aina gani?
▪ Abramu na mke wake waliishi katika jiji la Wakaldayo la Uru lenye ufanisi. Lakini kwa kutii agizo la Mungu, waliondoka katika jiji hilo na kuanza kuishi katika mahema. (Mwanzo 11:31; 13:12) Fikiria mambo ambayo huenda walihitaji kudhabihu ili kutii agizo hilo.
Uru, ambalo sasa ni eneo la Iraq ya kisasa, lilichimbuliwa na Leonard Woolley kati ya mwaka wa 1922 na 1934. Kati ya majengo aliyopata, kulikuwa na nyumba 73 zilizojengwa kwa matofali. Vyumba vingi katika nyumba hizo vilikuwa vimejengwa kuzunguka uga, au sehemu ya katikati iliyokuwa na sakafu ya mawe. Sakafu hiyo ilitengenezwa ikiwa imeinama kidogo kuelekea sehemu ya katikati, ambapo palikuwa na shimo la kuondolea maji machafu. Katika nyumba zilizokuwa kubwa kidogo, vyumba vya wageni vilikuwa na vyoo ndani. Chini ya vyumba vilivyokuwa juu kulikuwa na vyumba vya watumwa na vyumba vya kupikia vyenye majiko. Familia ilikaa katika vyumba vya juu na ilitumia ngazi kufika kwenye vyumba hivyo. Ngazi hizo zilimfikisha mtu kwenye roshani ya mbao iliyokuwa imejengwa kuzunguka uga. Walitembea kwenye roshani hiyo ili kufika kwenye milango ya vyumba hivyo vya juu.
“Nyumba . . . , yenye uga wa mawe na kuta zilizopakwa chokaa vizuri, yenye mfumo wa kuondolea maji machafu, . . . na vyumba 12 au zaidi, inaonyesha watu waliishi maisha ya juu sana,” akaandika Woolley. “Na hizo ndizo nyumba . . . zilizomilikiwa na watu wasio matajiri sana, wenye maduka, wafanyabiashara ndogondogo, waandishi, na wengineo.”
-
-
Je, Wajua?Mnara wa Mlinzi—2011 | Januari 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 19]
Mchoro wa nyumba katika siku za Aabrahamu
[Hisani]
© Drawing: A. S. Whitburn
-