Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • SUJATA mwenye umri wa miaka 18, ambaye ni wa familia ya Kihindu ya wala mboga, alikubaliana haraka na mashauri ya ulaji ya Mungu kwa mwanadamu wa kwanza, Adamu. Lakini akauliza mara moja: “Kwa nini, basi, watu huua wanyama kwa ajili ya chakula wakati kuna vitu vingine vingi sana vya kula?”

      Watu wengi kote ulimwenguni hujiuliza mambo haya. Mamia ya mamilioni katika Mashariki hula milo isiyo na nyama. Kwa kuongezea, idadi ya wala mboga katika Magharibi inaongezeka. Katika Marekani peke yake, karibu watu milioni 12.4 hudai kuwa wala mboga, karibu milioni 3 zaidi ya mwongo uliopita.

      Kwa nini watu wengi sana hupendelea ulaji usio na nyama? Ni nini maoni yanayofaa kuhusu uhai wa wanyama? Je, kula nyama huonyesha kutoheshimu uhai? Kulingana na yale yaliyoandikwa kwenye Mwanzo 1:29, je, ni vibaya kula nyama? Kwanza, fikiria kwa nini wengine hawali nyama.

      Kwa Nini Wengine Hawali Nyama?

      Kwa Sujata, ulaji wake huhusisha itikadi zake za kidini. “Nililelewa nikiwa Mhindu, nikiamini katika fundisho la kuzaliwa upya katika umbo jingine,” yeye aeleza. “Kwa kuwa nafsi ya kibinadamu yaweza kurudi ikiwa mnyama, nawaona wanyama kuwa sawa na mimi. Hivyo yaonekana kuwa vibaya kuwaua kwa chakula.” Dini nyinginezo pia hupendekeza ulaji wa mboga.

      Mambo mengine zaidi ya itikadi za kidini pia huathiri machaguo ya watu ya vyakula. Kwa kielelezo, Dakt. Neal Barnard, asisitiza hivi: “Sababu tu za kula nyama ni tabia au kutokujua.” Msimamo wake thabiti unategemea maoni yake kuhusu hatari za kiafya za kula nyama, kama vile maradhi ya moyo na kansa.a

      Katika Marekani, matineja wanasemekana kuwa sehemu inayokua haraka zaidi ya wala mboga. Sababu moja ikiwa hangaiko kwa wanyama. “Watoto hupenda wanyama,” asema Tracy Reiman wa shirika la Watu wa Kutetea Wanyama Watendewe Ifaavyo. “Waanzapo kujifunza juu ya linalowapata wanyama kabla hawajauawa kwa chakula inaongeza tu huruma wanayohisi.”

      Wengi wanaohangaikia mazingira pia hufahamu uhusiano uliopo kati ya ulaji wao na dai kubwa mno linalofanywa juu ya mali ya asili katika kulea wanyama kwa ajili ya chakula. Kwa kielelezo, inachukua karibu lita 3,300 za maji kutokeza kilogramu moja tu ya nyama ya ng’ombe na lita 3,100 kwa kilogramu moja ya nyama ya kuku. Kwa wengine, hii inakuwa sababu ya kuepuka nyama.

  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • Kuwa Wenye Huruma Kuelekea Wanyama

      Wala mboga wengine pia wana moyo mweupe wa kuhangaikia jinsi wanyama wanavyotendwa na biashara za kisasa za nyama. “Biashara ya mifugo haipendezwi na silika za kiasili za wanyama,” chataja kitabu The Vegetarian Handbook. “Wakifugwa katika vyumba vilivyosongamana vibaya na mazingira yasiyo ya asili,” kitabu hicho chasema, “wanyama wa siku hizi hutumiwa vibaya zaidi kuliko wanyama wa wakati mwingine wowote.”

      Ingawa Mungu hakatazi kutumia wanyama kwa chakula, anakataza kuwatenda kikatili. “Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake,” Biblia husema kwenye Mithali 12:10. Na Sheria ya Kimusa iliamuru wanyama watunzwe ifaavyo. — Kutoka 23:4, 5; Kumbukumbu la Torati 22:10; 25:4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki