Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • SUJATA mwenye umri wa miaka 18, ambaye ni wa familia ya Kihindu ya wala mboga, alikubaliana haraka na mashauri ya ulaji ya Mungu kwa mwanadamu wa kwanza, Adamu. Lakini akauliza mara moja: “Kwa nini, basi, watu huua wanyama kwa ajili ya chakula wakati kuna vitu vingine vingi sana vya kula?”

  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • Kwa Sujata, ulaji wake huhusisha itikadi zake za kidini. “Nililelewa nikiwa Mhindu, nikiamini katika fundisho la kuzaliwa upya katika umbo jingine,” yeye aeleza. “Kwa kuwa nafsi ya kibinadamu yaweza kurudi ikiwa mnyama, nawaona wanyama kuwa sawa na mimi. Hivyo yaonekana kuwa vibaya kuwaua kwa chakula.” Dini nyinginezo pia hupendekeza ulaji wa mboga.

  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • Wengine, kama Sujata, ambao huwaona wanyama kuwa sawa na wanadamu huhisi kwa nguvu kwamba kutoa uhai wa mnyama kwa sababu yoyote ni kosa — na hasa kuwaua kwa ajili ya chakula. Hata hivyo, Maandiko huonyesha kuwa Mungu hutofautisha kati ya uhai wa wanyama na uhai wa wanadamu nayo huruhusu uuaji wa wanyama kwa sababu mbalimbali. Kwa kielelezo, katika Israeli mnyama angeuawa ikiwa angekuwa tisho kwa uhai wa mwanadamu au mifugo ya mtu. — Kutoka 21:28, 29; 1 Samweli 17:34-36.

  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • Mwanamke mmoja Mhindu, mwenye umri wa miaka 70, alipoisoma Biblia kwa mara ya kwanza, alipata lile wazo la dhabihu za wanyama kuwa lisilopendeza. Lakini kadiri alivyoendelea katika ujuzi wake juu ya Maandiko, aliweza kuona kuwa dhabihu zilizoagizwa na Mungu zilikuwa na kusudi. Zilielekeza mbele kwenye dhabihu ya Yesu Kristo, ambayo ingetimiza takwa la kisheria kwa ajili ya msamaha wa dhambi. (Waebrania 8:3-5; 10:1-10; 1 Yohana 2:1, 2) Katika visa vingi yale matoleo yalitumika kama chakula kwa makuhani na nyakati nyingine kwa waabudu. (Mambo ya Walawi 7:11-21; 19:5-8) Mungu, ambaye kila kiumbe hai ni chake, angeweza kuweka kwa haki mpango kama huo kwa kusudi fulani. Bila shaka, Yesu alipokufa dhabihu za wanyama hazikuhitajika tena katika ibada. — Wakolosai 2:13-17; Waebrania 10:1-12.

  • Je, Ni Vibaya Kula Nyama?
    Amkeni!—1997 | Agosti 8
    • Kwa hakika, usadikisho wa Sujata juu ya wanyama ulitegemea itikadi katika lile fundisho la kuzaliwa upya katika umbo jingine. Kuhusu hili Biblia hueleza kwamba ingawa wanadamu na wanyama ni nafsi, nafsi si isiyoweza kufa. (Mwanzo 2:7; Ezekieli 18:4, 20; Matendo 3:23; Ufunuo 16:3) Wakiwa nafsi, wanadamu na wanyama hufa na hukoma kuwako. (Mhubiri 3:19, 20) Hata hivyo, wanadamu wana taraja la ajabu la ufufuo katika ulimwengu mpya wa Mungu.b (Luka 23:43; Matendo 24:15) Hili pia laonyesha kuwa wanyama hawako sawa na wanadamu.

      “Hata hivyo, kwa nini badiliko hilo katika ulaji?” Sujata alitaka kujua. Yaonekana tabia ya nchi ilibadilika sana kwa sababu ya Furiko. Iwe Yehova aliongeza mlo wa nyama katika ulaji wa mwanadamu kwa sababu alitazamia mahitaji ya vizazi vya wakati ujao ambavyo vingeishi katika sehemu ambazo mboga zingekuwa chache, Biblia haisemi. Lakini Sujata angeweza kukubali kwamba Mmiliki wa vitu vyote vilivyo hai alikuwa na haki ya kuleta badiliko.

      Kuonyesha Staha kwa Ajili ya Uhai wa Wanyama

      Lakini, Sujata alistaajabu, ‘Hatupaswi angalau kuonyesha staha kwa uhai wa wanyama?’ Ndiyo, twapaswa. Na Muumba wa vitu vyote ametuambia tuwezavyo kufanya hivyo. “Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile,” lasema agizo lake kwenye Mwanzo 9:4. Kwa nini kuna katazo juu ya kula damu? “Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu,” Biblia husema. (Mambo ya Walawi 17:10, 11) Yehova ameweka masharti: ‘Imwageni damu ya mnyama aliyechinjwa juu ya nchi kama maji.’—Kumbukumbu la Torati 12:16, 24.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki