-
Je! Jina Lako Limo Katika Kitabu cha Uhai?Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Yeye ambaye hushinda atapambwa hivyo mavazi ya nje meupe; na mimi kwa njia yoyote sitafuta jina lake kutoka kitabu cha uhai, bali mimi nitakiri jina lake mbele za Baba yangu na mbele ya malaika zake.” (Ufunuo 3:4, 5, NW)
-
-
Je! Jina Lako Limo Katika Kitabu cha Uhai?Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
13. Ni baraka gani zilizo akibani kwa Wakristo wapakwa-mafuta ambao ‘hawachafui mavazi yao ya nje’?
13 Wale katika Sardisi ambao ni waaminifu mpaka mwisho na hawachafui utambulisho wao wa Kikristo wanafikia utimizo wa tumaini zuri ajabu. Baada ya kusimamishwa kwa Ufalme wa Kimesiya katika 1914, wanafufuliwa kwenye uhai wa kiroho na wakiwa washindi hupambwa mavazi meupe ya nje yakiwa ufananisho wa uadilifu wao usio na kasoro, wala waa. Wakiwa wamekwisha tembea katika ile njia yenye kusonga iongozayo kwenye uhai, watafurahia thawabu ya milele.—Mathayo 7:14; Ona pia Ufunuo 6:9-11.
Milele Katika Kitabu cha Uhai!
14. Kitabu cha uhai ni nini, na ni majina ya akina nani yaliyorekodiwa humo?
14 “Kitabu cha uhai,” ni nini na ni majina ya akina nani yatakayotunzwa humo? Kitabu, au hati-kunjo, cha uhai hurejezea rekodi ya watumishi wa Yehova wanaokuja katika mstari wa kupokea tuzo la uhai wa milele. (Malaki 3:16) Humu katika Ufunuo rejezo mahususi limefanywa kwenye majina ya Wakristo wapakwa-mafuta. Lakini majina ya wale walio katika mstari wa uhai wa milele duniani yamerekodiwa pia humo. Zaidi ya hilo, majina yanaweza ‘kufutwa’ katika kitabu hicho. (Kutoka 32:32, 33) Hata hivyo, wale wa jamii ya Yohana ambao majina yao yanabaki katika kile kitabu cha uhai mpaka kifo chao wanapokea uhai usioweza kufa katika mbingu. (Ufunuo 2:10) Haya ndiyo majina ambayo Yesu anakiri hasa mbele za Baba yake na mbele ya malaika Zake. Lo! ni kubwa mno jinsi gani thawabu hiyo!
-