-
Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya UshindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Hawa ndio ambao hawakujichafua wenyewe na wanawake; kwa kweli, wao ni mabikira. Hawa ndio ambao hufuliza kufuata Mwana-Kondoo si kitu aenda wapi. Hawa walinunuliwa kutoka miongoni mwa aina ya binadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana-Kondoo,
-
-
Kuimba Wimbo Mpya wa Sherehe ya UshindiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Uhakika wa kwamba 144,000 “ni mabikira” haumaanishi kwamba washiriki wa jamii hii kwa lazima ni wasiooa na wasioolewa katika mnofu. Mtume Paulo aliandikia Wakristo ambao walikuwa na mwito wa kimbingu kwamba, ingawa kuna faida katika useja wa Kikristo, ndoa ni afadhali katika hali fulani. (1 Wakorintho 7:1, 2, 36, 37) Kinachoainisha jamii hii ni ubikira wa kiroho. Wao wameepuka uzinzi wa kiroho pamoja na siasa za kilimwengu na pamoja na dini bandia. (Yakobo 4:4; Ufunuo 17:5) Wakiwa bibi-arusi aliyeposwa na Kristo, wao wamejiweka wenyewe safi, “wakiwa bila waa miongoni mwa kizazi kombo na chenye kupopotolewa.”—Wafilipi 2:15, NW.
-