Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Kuvurumisha Moto Kwenye Dunia

      6. Kunakuwa na nini baada ya hicho kimya katika mbingu, na ni katika kuitikia nini?

      6 Yohana anatuambia: “Lakini mara hiyo malaika akachukua chombo cha uvumba, na kukijaza baadhi ya moto wa madhabahu na kuuvurumisha kwenye dunia. Na ngurumo zikatukia na sauti na meme na tetemeko la dunia.” (Ufunuo 8:5, NW) Baada ya kimya, kuna utendaji wa ghafula wenye kutazamisha! Kwa wazi huo ni katika kuitikia “sala za watakatifu,” kwa kuwa huo unaanzishwa na moto uliochukuliwa kutoka madhabahu ya uvumba. Huko nyuma katika 1513 K.W.K. kwenye Mlima Sinai, ngurumo na meme, kelele kubwa, moto, na kutetemeka kwa mlima viliashiria kugeuzwa kwa uangalifu wa Yehova kuelekea watu wake. (Kutoka 19:16-20) Madhihirisho kama hayo yanayoripotiwa na Yohana hali kadhalika huonyesha uangalifu wa Yehova ukitolewa kwa watumishi wake duniani. Lakini anachoona Yohana kinatolewa kwa ishara. (Ufunuo 1:1, NW) Kwa hiyo moto, ngurumo, sauti, meme, na tetemeko la dunia vya ufananisho vitafasiriwaje leo?

  • Tauni za Yehova juu ya Jumuiya ya Wakristo
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 8, 9. (a) J. F. Rutherford alielezaje habari ya mwelekeo na tamaa ya watu wa Mungu wakati wa miaka migumu ya vita? (b) Ilikuwaje kwamba moto ulivurumishwa kwenye dunia? (c) Ngurumo, sauti, meme, na tetemeko la dunia vimetukiaje?

      8 Akirejezea magumu ya karibuni ya watu wa Mungu, mhutubu huyo alisema: “Shambulio la adui lilikuwa lisilo na sikitikio sana hivi kwamba wengi wa kundi lenye kupendwa la Bwana waliduwaa wakasimama tuli kwa mshangao, wakisali na kungojea Bwana aonyeshe penzi lake. . . . Lakini ijapokuwa kivunja-moyo cha kitambo, kulikuwako tamaa yenye kuwaka ya kutangaza ujumbe wa ufalme.”—Ona toleo la Septemba 15, 1919 la The Watch Tower ukurasa 280.

      9 Katika 1919 tamaa hiyo ilitoshelezwa. Hiki kikundi kidogo lakini chenye kutenda cha Wakristo kiliwashwa moto, kusema kiroho, waanze kampeni ya kuhubiri ulimwenguni pote. (Linga 1 Wathesalonike 5:19.) Moto ulivurumishwa duniani katika njia ya kwamba Ufalme wa Mungu ukawa ndilo suala lenye kuwaka, na ndivyo unaendelea kuwa! Sauti zenye nguvu zilichukua mahali pa kimya, zikivumisha ujumbe wa Ufalme kwa uwazi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki