-
Misaada Yatolewa Kotekote DunianiAmkeni!—2001 | Julai 22
-
-
Ijapokuwa wakurugenzi, mameneja, na wasimamizi wengi wanahisi kwamba wafanyakazi waliojitolea ni watu wa “maana sana,” bado hawaonyeshi uthamini kwa kazi wanayofanya. Ili kubadili hali hiyo, shirika la Umoja wa Mataifa liliamua kutilia mkazo umuhimu wa wafanyakazi wa kujitolea katika mwaka huu wa 2001. Sanduku “Mwaka wa Kimataifa wa Wafanyakazi wa Kujitolea” laonyesha malengo mbalimbali ambayo shirika la Umoja wa Mataifa latazamia kutimiza.
-
-
Misaada Yatolewa Kotekote DunianiAmkeni!—2001 | Julai 22
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 5]
Mwaka wa Kimataifa wa Wafanyakazi wa Kujitolea
Katika Novemba 20, 1997, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza mwaka wa 2001 kuwa “Mwaka wa Kimataifa wa Wafanyakazi wa Kujitolea.” Shirika la Umoja wa Mataifa lataka malengo manne yatimizwe mwaka huu.
Kutoa shukrani Serikali zinahimizwa zitambue umuhimu wa wafanyakazi wa kujitolea kwa kuchunguza na kurekodi kile wanachotimiza na kutoa tuzo kwa utendaji wao bora.
Kutunga sheria zinazoendeleza kazi ya kujitolea Serikali zinahimizwa zichochee watu kujitolea, kwa mfano, kwa kukubali watu wafanye kazi ya kujitolea badala ya kufanya utumishi wa kijeshi au kuwapunguzia kodi fulani zinazotozwa na serikali.
Kutumia vyombo vya habari Vyombo vya habari vimekaribishwa kusaidia kuchapisha na kutangaza habari za miradi iliyofanikiwa ya kazi ya kujitolea. Kwa njia hiyo wengine wangeweza kuiga miradi hiyo iliyofanikiwa, na “jumuiya nyingine hazingehitaji kutumia muda mrefu na kujitahidi kuunda miradi yake yenyewe.”
Kutangaza faida zake Mashirika ya wafanyakazi wa kujitolea yanahimizwa yapange maonyesho ili kujulisha watu juu ya jinsi ambavyo jamii hunufaika kwa kazi ya kujitolea.
Shirika la Umoja wa Mataifa latumaini kwamba watu wengi zaidi watatiwa moyo kuomba msaada wa wale waliojitolea na watu wengi zaidi watajitolea kufanya kazi katika mwaka wa 2001, ambao ni Mwaka wa Kimataifa wa Wafanyakazi wa Kujitolea. Mbali na hayo, ili mashirika ya wafanyakazi wa kujitolea yaweze kushughulikia mahitaji yanayoongezeka ya jamii, mahali pengi zaidi pa kufanyia kazi huhitajika na vilevile fedha nyingi zaidi. Serikali 123 zimekubali kugharimia malengo ya azimio hilo la Umoja wa Mataifa.
-