Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 26. Kuna ithibati gani ya hatia ya damu upande wa Babuloni Mkubwa?

      26 Kwa muda wa karne zilizopita, milki ya ulimwengu ya dini bandia imemwaga damu nyingi kama bahari. Mathalani, katika Japani ya zamani za kale, mahekalu katika Kyoto yaligeuzwa kuwa ngome, na watawa-mashujaa-vita, wakiliitia “jina takatifu la Buddha,” walipigana vita mpaka barabara zikawa nyekundu kwa damu. Katika karne ya 20, viongozi wa kidini walipiga miguu wakiwa pamoja na majeshi ya nchi zao, na walichinjana, kukiwa na hasara ya angalau maisha milioni mia moja.

  • Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa Mbaya
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 238]

      Chini ya kichwa hiki, makala inayofuata ilitokea katika chapa ya kwanza ya The New York Times ya Desemba 7, 1941:

      ‘SALA YA VITA’ KWA AJILI YA REICH

      Maaskofu wa Kikatoliki katika Fulda Waomba Baraka na Ushindi

      Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujeremani lililokusanyika katika Fulda limependekeza ianzishwe ‘sala ya vita’ maalumu ambayo itasomwa mwanzoni na mwishoni mwa ibada zote za kimungu. Sala hiyo husihi Mungu abariki silaha za Ujeremani kwa ushindi na kutoa himaya kwa maisha na afya ya askari-jeshi wote. Maaskofu hao waliwaagiza zaidi makasisi wa Kikatoliki waweke na kukumbuka katika mahubiri maalumu ya Jumapili angalau mara moja kwa mwezi askari-jeshi Wajeremani ‘barani, baharini na hewani.’”

      Makala hii iliondolewa kwenye chapa za baadaye za nyusipepa hiyo. Desemba 7, 1941, ndiyo siku Japani, nchi fungamani na Ujeremani, iliposhambulia meli za U.S. kwenye Pearl Harbor.

      [Picha katika ukurasa wa 244]

      “Majina ya Kufuru”

      Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alipoendeleza Ushirika wa Mataifa baada ya Vita ya Ulimwengu 1, hawara zake wa kidini walitafuta mara hiyo kulipa tendo hilo idhini ya kidini. Kama tokeo, tengenezo jipya la amani ‘likajawa na majina ya kufuru.’

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki