-
Safari yenye Msiba ya Manowari za HispaniaAmkeni!—2007 | Agosti
-
-
Safari yenye Msiba ya Manowari za Hispania
NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI HISPANIA
ZAIDI ya miaka mia nne iliyopita, vikosi viwili vya wanamaji vilipigana katika Mlango-Bahari wa Uingereza. Vita hivyo kati ya Waprotestanti na Wakatoliki vilikuwa sehemu ya mapambano yaliyotokea katika karne ya 16 kati ya majeshi ya Malkia Mprotestanti Elizabeth wa Kwanza wa Uingereza na Mfalme Mkatoliki Philip wa Pili wa Hispania. Kitabu The Defeat of the Spanish Armada kinaeleza hivi: “Kwa maoni ya watu waliokuwa wakiishi wakati huo, vita hivyo kati ya majeshi ya wanamaji wa Uingereza na Hispania katika Mlango-Bahari wa Uingereza vilikuwa mapambano ya kufa na kupona kati ya majeshi ya nuru na majeshi ya giza.”
-
-
Safari yenye Msiba ya Manowari za HispaniaAmkeni!—2007 | Agosti
-
-
Kwa Nini Walijaribu Kuvamia?
Kwa miaka mingi, maharamia Waingereza walipora meli za Hispania, na Malkia Elizabeth wa Uingereza aliunga mkono kwa dhati uasi wa Uholanzi dhidi ya utawala wa Hispania. Isitoshe, Mfalme Mkatoliki Philip wa Pili aliona kuwa ni jukumu lake kuwasaidia Waingereza Wakatoliki waondolee mbali harakati ya Waprotestanti ambao waliiona kuwa “uasi.” Kwa sababu hiyo, Manowari za Hispania zilikuwa na makasisi na washauri wa kidini 180 hivi. Majeshi ya Manowari yalipokusanyika, kila mtu aliungama dhambi zake kwa kasisi na akala Sakramenti.
Hali ya kidini nchini Hispania na ya mfalme wa nchi hiyo ilionekana wazi katika maneno haya ya Mjesuti Mhispania Pedro de Ribadeneyra: “Mungu Bwana wetu, atatutangulia kwa sababu tunatetea imani na kusudi lake takatifu. Tukiwa na kapteni kama huyo hatuogopi chochote.” Kwa upande mwingine, Waingereza walitumaini kwamba ikiwa wangeshinda vita hivyo Uprotestanti ungeenea katika bara lote la Ulaya.
-