-
Faida za Kutembelea Majumba ya UkumbushoAmkeni!—2005 | Machi 8
-
-
Jumba la Ukumbusho la Pekee
Bila shaka, watalii wengi huvutiwa hasa na Taasisi ya Smithsonian. Kwa nini? Ni kwa sababu taasisi hiyo ina majumba kadhaa ya ukumbusho na vituo vya elimu. Unaweza kuona kwa urahisi Kasri ya Smithsonian iliyo katika National Mall, ambalo ni eneo lenye nyasi na lenye urefu wa kilometa 1.5. Jengo la Capitol liko mwanzoni mwa eneo hilo huku Nguzo ya Washington ikiwa mwishoni mwake. Ikiwa utasimama kuelekeana na Nguzo ya Washington, unaweza kuona Kasri ya Smithsonian, ambalo ni jengo muhimu la mawe lenye rangi nyekundu lililoko upande wa kushoto wa eneo hilo maarufu.
Ni jengo gani lililo muhimu zaidi katika Taasisi ya Smithsonian? Katika enzi hii ya sayansi, jengo muhimu zaidi ni Jumba la Ukumbusho la Kitaifa la Usafiri wa Anga, ambalo kulingana na kitabu kimoja cha wasafiri, “ndilo jumba la ukumbusho linalotembelewa sana ulimwenguni.” Kwa nini watu wengi huvutiwa na jumba hilo? Jumba hilo lina sehemu 23 za maonyesho. Vitu vilivyomo huonyesha mambo yanayosisimua kuhusu historia ya usafiri wa anga. Vitu vingi katika jumba hilo vimening’inizwa darini. Katika sehemu ya maonyesho inayoitwa Milestones of Flight kuna ndege inayoitwa Flyer, ambayo Orville Wright alitumia katika safari yake maarufu ya mwaka wa 1903 huko Kitty Hawk, North Carolina. Karibu nayo, kuna ndege inayoitwa Spirit of St. Louis, ambayo Charles Lindbergh alitengeneza ili ashinde tuzo ya kuwa mtu wa kwanza kuvuka Bahari ya Atlantiki kwa ndege akiwa peke yake katika mwaka wa 1927. Isitoshe, katika jumba hilo la ukumbusho kuna vyombo vya angani vilivyo maarufu ambavyo vimetumiwa karibuni na vilevile mawe yaliyotolewa mwezini.
-
-
Faida za Kutembelea Majumba ya UkumbushoAmkeni!—2005 | Machi 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 14]
Kasri ya Smithsonian
[Hisani]
Smithsonian photo by Eric Long
[Picha katika ukurasa wa 14, 15]
Jumba la Ukumbusho la Kitaifa la Usafiri wa Anga lina ndege ya “Flyer” ya mwaka wa 1903 (kulia) na ndege ya Lindbergh inayoitwa “Spirit of Saint Louis” (chini)
-