Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Faida za Kutembelea Majumba ya Ukumbusho
    Amkeni!—2005 | Machi 8
    • Jumba la Ukumbusho la Utamaduni wa Waamerika

      Jumba hilo jipya zaidi kati ya majumba ya ukumbusho ya Taasisi ya Smithsonian linawakumbusha watu kuhusu wakaaji wa zamani zaidi wa mabara ya Amerika. Jamii zaidi ya 500 za Wenyeji wa Asili wa Amerika waliishi katika mabara hayo kabla Wazungu na Waafrika hawajafika huko. Hilo huitwa Jumba la Ukumbusho la Kitaifa la Wahindi Waamerika nalo liko katika eneo la National Mall, karibu na Jumba la Ukumbusho la Usafiri wa Anga. Jumba hilo lilifunguliwa mnamo Septemba 21, 2004. Ni rahisi kulitambua jengo hilo kwani lina mistari ya pekee iliyopindika. Kuta za nje za jengo hilo lenye ukubwa wa meta 23,000 za mraba, zimefunikwa kwa chokaa ya Kasota kutoka Minnesota. Jengo hilo linafanana na “mwamba wenye matabaka mengi uliochongwa kwa pepo na maji.”

      Unafikiri kuna nini humo? Sehemu tano kuu za maonyesho zina “vitu 7,000 hivi kati ya vitu 800,000 vya kiakiolojia na kitamaduni vinavyopatikana katika Jumba la Ukumbusho la Kitaifa la Wahindi Waamerika.” (Insight, gazeti la Smithsonian) Kuna vikapu, vyombo vya udongo, na shanga zilizotengenezwa na kabila la Mapuche nchini Chile, kabila la Quechua nchini Peru, kabila la Lakota nchini Marekani, na kabila la Anishinabe nchini Kanada.

      Mwanzilishi wa jumba hilo, W. Richard West, Jr., ambaye ni Mcheyenne wa Kusini, anasema kwamba kusudi la jumba hilo ni “kurekebisha maoni mabaya na kuwasaidia watu wote, yaani wenyeji na wale ambao si wenyeji, kuelewa maisha na utamaduni wa wenyeji wa mabara hayo.” Inachukua saa mbili hivi kutembea na kuona vitu vya utamaduni wa Wahindi Waamerika.

  • Faida za Kutembelea Majumba ya Ukumbusho
    Amkeni!—2005 | Machi 8
    • [Picha katika ukurasa wa 18]

      Jumba la Ukumbusho la Kitaifa la Wahindi Waamerika lina muundo wa pekee wa mistari iliyopindika

      [Hisani]

      Photo by Robert C. Lautman

      [Picha katika ukurasa wa 18]

      Chombo cha glasi kilichotengenezwa na msanii wa kisasa ambaye ni Mhindi Mwamerika

      [Hisani]

      Photo by Ernest Amoroso, © Smithsonian Institution/National Museum of the American Indian

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki