Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kutumikia Pamoja na Mlinzi
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Januari 1
    • 14. Jamii ya mlinzi ya Yehova imetumia gazeti gani kwa njia yenye kutokeza, na Yehova amebarikije utumizi wake?

      14 Nyakati zote jamii ya mlinzi imefanya kazi yake kwa bidii ikiwa na hamu kubwa ya kufanya lililo jema. Mwezi wa Julai 1879, Wanafunzi wa Biblia walianza kuchapisha gazeti hili, ambalo wakati huo liliitwa Zion’s Watch Tower and Herald of Christ’s Presence. Kila toleo tangu mwaka wa 1879 hadi Desemba 15, 1938, lilikuwa na maneno haya kwenye jalada la mbele “‘Ee Mlinzi, Habari Gani za Usiku?’—Isaya 21:11.”a Kwa miaka 120, gazeti la Mnara wa Mlinzi limekuwa likilinda kwa uaminifu juu ya matukio ya ulimwengu na maana yake ya unabii. (2 Timotheo 3:1-5, 13)

  • Kutumikia Pamoja na Mlinzi
    Mnara wa Mlinzi—2000 | Januari 1
    • “Mlinzi” Akaa Macho

      12. Ni nani leo walio jamii ya mlinzi, nao wamekuwa na mtazamo gani?

      12 Basi, “wakati wa mwisho” ulipoanza, mara nyingine tena Yehova akamtokeza mlinzi, anayewatolea watu onyo juu ya matukio yahusuyo utimizo wa makusudi Yake. (Danieli 12:4; 2 Timotheo 3:1) Hadi leo hii, jamii hiyo ya mlinzi—Wakristo watiwa-mafuta, Israeli wa Mungu—imekuwa ikitenda kupatana na ufafanuzi wa unabii wa Isaya kuhusu mlinzi: “[Alisikiliza] sana, akijitahidi kusikiliza. Ndipo akalia kama simba, Ee Bwana, mimi nasimama daima juu ya mnara wakati wa mchana, na kila usiku ninakaa katika zamu ya ulinzi wangu.” (Isaya 21:7, 8) Huyo ni mlinzi anayechukua kazi yake kwa uzito!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki