-
Urusi2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
Kulikuwa na njia nyingine za kulinda chakula cha kiroho. Aleksey Nepochatov anasema hivi: “Ndugu fulani waliweza kuandika kwa mwandiko mdogo kama utando wa buibui. Ncha ya kalamu ilichongwa na kuwa nyembamba sana hivi kwamba kwenye mstari mmoja wa karatasi mtu angeweza kuandika mistari mitatu au minne ya maandishi. Kasha dogo la kiberiti lingeweza kuwekwa nakala tano au sita za Mnara wa Mlinzi zilizoandikwa kwa mwandiko huo mdogo. Ili kuweza kuandika kwa mwandiko huo, mtu alihitaji kuwa na macho mazuri sana na alipaswa kuwa mvumilivu. Baada ya taa zote kuzimwa na watu wote kulala, ndugu hao waliandika wakiwa wamejifunika blanketi. Walitumia mwangaza wa taa iliyokuwa kwenye lango la kambi ambayo haikuwa inafanya kazi vizuri. Mtu alipofanya kazi hiyo kwa miezi kadhaa macho yake yaliharibika. Mara nyingine mlinzi angegundua, na ikiwa alitupenda angesema, ‘Bado mnaandika-andika tu, mtalala saa ngapi?’”
-
-
Urusi2008 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
-
-
[Picha katika ukurasa wa 175]
Kasha dogo la kiberiti lingeweza kuwekwa nakala tano au sita za “Mnara wa Mlinzi” zilizoandikwa kwa mwandiko mdogo
-