-
Je, Maisha Yako Yanaweza Kuwa na Maana Zaidi?Mnara wa Mlinzi—2000 | Julai 15
-
-
THAMANI ya kweli haiamuliwi kwa macho tu. Noti yenye thamani kubwa zaidi katika Marekani ilikuwa ya dola 10,000. Lakini karatasi ya noti hiyo ni yenye thamani ndogo.
Je, umewahi kujiuliza kama karatasi hizo ambazo hazina thamani zinaweza kufanya maisha yako yawe na maana ya kweli? Watu wengi hufikiri hivyo. Mamilioni ya watu hufanya kazi mchana na usiku ili kuchuma fedha nyingi kadiri wawezavyo. Nyakati nyingine kufuatia fedha huwalazimu wadhabihu afya yao, rafiki zao, na hata familia zao. Kwa mafanikio gani? Je, fedha—au vitu vinavyonunuliwa na fedha—vinaweza kutupa uradhi wa kweli na wa kudumu?
Kulingana na wachunguzi, kadiri tutafutavyo uradhi unaoletwa na mali, ndivyo inavyoonekana kuwa vigumu kuupata. Mwandishi mmoja wa habari, Alfie Kohn atoa kauli ya kwamba “kwa wazi uradhi haununuliwi. . . . Watu ambao utajiri ndio jambo kuu maishani mwao huelekea kupatwa na mahangaiko kupita kiasi na mshuko wa moyo pamoja na kukosa afya kwa ujumla.”—International Herald Tribune.
-
-
Jinsi Maisha Yako Yanavyoweza Kuwa na Maana ZaidiMnara wa Mlinzi—2000 | Julai 15
-
-
MITHALI moja ya kale husema hivi: “Usijitaabishe ili kupata utajiri; acha kuzitegemea akili zako mwenyewe. Je! utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, kama tai arukaye mbinguni.” (Mithali 23:4, 5) Yaani, si jambo la hekima kujichosha tukijaribu kuwa matajiri, kwa kuwa utajiri waweza kuruka kana kwamba umebebwa kwenye mabawa ya tai.
Kama ionyeshavyo Biblia, utajiri waweza kutokomea upesi. Unaweza kutoweka kwa usiku mmoja kwa sababu ya misiba ya asili, hali mbaya ya kiuchumi, au matukio mengine yasiyotazamiwa. Zaidi ya hayo, hata wale ambao wamepata ufanisi wa kimwili mara nyingi huwa wametamauka. Fikiria kisa cha John, ambaye kazi yake ilitia ndani kuwatumbuiza wanasiasa, wanamichezo mashuhuri, na watawala.
John ataarifu hivi: “Nilikaza fikira zangu zote katika kazi yangu. Nikawa tajiri sana, nikalala katika hoteli za hali ya juu, na hata wakati mwingine nilisafiri kwenda kazini kwa ndege yangu. Mwanzoni nilifurahia hali hiyo, lakini pole kwa pole nikachoshwa. Watu wale niliowahudumia walionekana wakichukua mambo kijuujuu tu. Maisha yangu hayakuwa na maana.”
-