Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yule Mwanamke Tasa Ashangilia
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA.”—Isaya 54:16, 17.

  • Yule Mwanamke Tasa Ashangilia
    Unabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
    • Kwa hiyo leo, hata kama majeshi yaliyo na nguvu zaidi ulimwenguni yatawashambulia watu wa Yehova, hayataweza kupata mafanikio kamili. Kwa nini hayataweza?

      27, 28. Tunaweza kuwa na uhakika wa jambo gani katika nyakati hizi zenye msukosuko, na ni kwa nini tunajua kwamba mashambulio ya Shetani juu yetu hayatafanikiwa?

      27 Wakati wa kufanya shambulio la uharibifu juu ya watu wa Mungu na ibada yao ya roho na kweli umekwisha. (Yohana 4:23, 24) Yehova alimruhusu Babiloni Mkubwa afanye shambulio moja lililofanikiwa kwa muda. Kwa muda mfupi, “Yerusalemu la juu” liliona wazao wake wakikaribia kunyamazishwa wakati kazi ya kuhubiri duniani ilipokaribia kukomeshwa kabisa. Hilo halitatukia tena ng’o! Sasa jiji hilo linawashangilia wana wake, kwani hawawezi kushindwa kiroho. (Yohana 16:33; 1 Yohana 5:4) Ni kweli kwamba silaha za ushambulizi zimeundwa kuwapinga, na bado zitaundwa. (Ufunuo 12:17) Lakini silaha hizo hazijafaulu na hazitafaulu. Shetani hana silaha yoyote ya kuizima imani na bidii motomoto ya watiwa-mafuta na waandamani wao. Amani hii ya kiroho ndio ‘urithi wa watumishi wa Yehova,’ kwa hiyo hakuna mtu anayeweza kuwapokonya amani hiyo.—Zaburi 118:6; Waroma 8:38, 39.

      28 Ndiyo, ulimwengu wa Shetani hauna kamwe kitu kitakachoweza kuikomesha kazi na ibada safi ya daima ambayo Mungu anapewa na watumishi wake waliojiweka wakfu. Wazao watiwa-mafuta wa “Yerusalemu la juu” wamefarijiwa sana na uhakikisho huo. Na umewafariji pia washiriki wa ule umati mkubwa. Tunapozidi kujua mengi juu ya tengenezo la Yehova la kimbingu na jinsi linavyoshughulika na waabudu wa Yehova duniani, imani yetu itazidi kuwa yenye nguvu. Maadamu imani yetu ina nguvu, silaha za Shetani zitakuwa za bure kabisa zinapotumiwa kupigana nasi!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki