Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Karne ya Ujeuri
    Amkeni!—2002 | Mei 8
    • Silaha za kibiolojia na za kemikali. Kupigana kwa kutumia vijidudu huhusisha matumizi ya bakteria hatari au virusi, kama vile bakteria ya kimeta au virusi vya ndui. Ndui ni hatari sana kwani watu huambukizwa ugonjwa huo kwa urahisi. Pia kuna silaha za kemikali, kama vile gesi ya sumu. Kuna aina nyingi za silaha za kemikali, na ijapokuwa zimepigwa marufuku kwa miaka mingi, zingali zinatumiwa.

      Je, silaha hizo kali na madhara yanayosababishwa nazo zimewafanya watu ‘waogope na kuvunja majeshi yao,’ kama vile Nobel alivyotabiri? Sivyo hata kidogo, kwani zimewafanya watu waogope sana wakifikiri kwamba huenda zikatumiwa siku moja—hata na watu wasiojua kuzitumia. Zaidi ya miaka kumi iliyopita, mkurugenzi wa Shirika la Marekani la Kudhibiti na Kupunguza Silaha alisema hivi: “Silaha za kemikali zinaweza kuundwa na mtu yeyote katika gereji lake, maadamu amejifunza mambo machache kuhusu kemia katika shule ya sekondari.”

  • Karne ya Ujeuri
    Amkeni!—2002 | Mei 8
    • [Picha katika ukurasa wa 7]

      Watu wengi walitambua jinsi silaha za kemikali zilivyo hatari wakati gesi ya “sarin” ilipotumiwa kwenye njia ya magari-moshi yanayopita chini ya ardhi huko Tokyo mnamo mwaka wa 1995

      [Hisani]

      Asahi Shimbun/Sipa Press

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki