Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Silaha Ndogondogo, Matatizo Makubwa
    Amkeni!—2001 | Machi 22
    • Mapigano Yanapokoma

      Mapigano yanapokoma, mara nyingi bunduki zilizotumika huingia mikononi mwa wahalifu. Fikiria juu ya nchi moja ya kusini mwa Afrika ambamo harakati za kisiasa zenye jeuri ziligeuka kuwa uhalifu wenye jeuri. Watu wapatao 10,000 walikufa kwa muda wa miaka mitatu tu kutokana na jeuri ya kisiasa. Mzozo huo ulipokoma, jeuri ya uhalifu iliibuka. Mashindano kati ya madereva wa teksi yalisababisha “mapigano ya teksi,” ambapo majambazi walikodiwa kuwapiga risasi abiria na madereva wa teksi za makampuni ya wapinzani. Mara nyingi, bunduki za kijeshi zilitumiwa katika wizi na uhalifu mwingineo. Katika mwaka mmoja wa hivi karibuni, watu 11,000 waliouawa kwa bunduki nchini humo, ikawa nchi ya pili ulimwenguni isiyo na vita kuwa na kiwango kikubwa hivyo.

      Kujua kwamba wahalifu wana silaha hatari hutokeza hofu na wasiwasi. Katika nchi nyingi zinazositawi, matajiri huishi katika nyumba zilizo kama ngome, zenye kuzingirwa na kuta na ua wa umeme na kulindwa na askari usiku na mchana. Wakazi wa nchi zilizositawi pia hutahadhari. Hilo limethibitika kuwa kweli hata katika maeneo ambayo hayajakumbwa na mizozo ya raia.

  • Silaha Ndogondogo, Matatizo Makubwa
    Amkeni!—2001 | Machi 22
    • Majeshi yanayopunguza askari wake huwapa majeshi mengine makumi ya mamilioni ya silaha bila malipo, au huagizwa kutoka sehemu ambazo mapigano yamekoma. Katika nchi fulani, bunduki zinapatikana kwa wingi hivi kwamba huuzwa kwa bei ndogo ya dola sita za Marekani au kubadilishwa kwa mbuzi, kuku au furushi la nguo kuukuu.

  • Silaha Ndogondogo, Matatizo Makubwa
    Amkeni!—2001 | Machi 22
    • Baada ya Vita Baridi kukoma, majeshi ya Mashariki na Magharibi yalipunguza wanajeshi na kuuza silaha za ziada au kuzitoa bure kwa serikali za nchi rafiki. Kwa mujibu wa mwandishi mmoja wa Taasisi ya Utafiti wa Amani huko Oslo, Norway, tangu mwaka wa 1995 nchi ya Marekani pekee imetoa bila malipo bunduki, bastola, bunduki ya rasharasha, na vyombo vya kurusha makombora zaidi ya 300,000. Inadhaniwa kwamba ni rahisi zaidi kutoa silaha bila malipo kuliko kuziharibu au kuziweka katika bohari na kuzilinda. Wachunguzi fulani wanakadiria kwamba silaha ndogondogo na silaha nyepesi zenye thamani ya dola bilioni tatu hivi za Marekani huvuka kihalali mipaka ya nchi mbalimbali kila mwaka.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki