-
Karne ya UjeuriAmkeni!—2002 | Mei 8
-
-
Mabomu ya ardhini. Kufikia mwisho wa karne ya 20, mabomu ya ardhini yalikuwa yakiwalemaza watu 70 hivi kwa wastani kila siku! Wengi waliolemazwa walikuwa raia, bali si wanajeshi. Mara nyingi, mabomu ya ardhini hayatumiwi kuua, bali hutumiwa kulemaza na kuwatisha watu wanaoathiriwa nayo.
Ni kweli kwamba jitihada nyingi zimefanywa katika miaka ya hivi majuzi kuondoa mabomu ya ardhini. Lakini watu fulani wanasema kwamba kwa kila bomu moja linaloondolewa, mabomu mengine 20 hutegwa na kwamba huenda ikawa kuna mabomu milioni 60 yaliyofukiwa ardhini ulimwenguni pote. Ingawa mabomu ya ardhini hayawezi kutofautisha kati ya mwanajeshi na mtoto anayecheza karibu na eneo lililotegwa, bado silaha hizo hatari zinaendelea kuundwa na kutumiwa.
-
-
Karne ya UjeuriAmkeni!—2002 | Mei 8
-
-
[Picha katika ukurasa wa 6]
Watu waliojeruhiwa na mabomu ya ardhini huko Kambodia, Iraq, na Azerbaijan
[Hisani]
UN/DPI Photo 186410C by P.S. Sudhakaran ▼
UN/DPI Photo 158314C by J. Isaac
UN/DPI Photo by Armineh Johannes
-