Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mwanzoni, Paul na Frances waliishi pamoja na familia ya Mufaulu Galuvao, lakini John na Helen Rhodes walipofika mwaka wa 1977, walihamia makao mapya ya wamishonari yaliyokuwa yamekodiwa huko Vaiala, Apia.

  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • KUZOEA MAISHA YA KISIWANI

      Kwa miaka mingi, Mashahidi wa nchi nyingine waliohamia Samoa walitambua kwamba hata kisiwa hicho maridadi kina matatizo yake. Mojawapo ya matatizo hayo ni usafiri. John Rhodes anasema: “Miaka miwili ya kwanza tuliyokaa Apia, mara nyingi tulitembea kwa muda mrefu ili kuhudhuria mikutano na kwenda kuhubiri. Nyakati nyingine tulisafiri kwa mabasi ya umma yenye madoido.”

      Kwa kawaida mabasi huwa na kichwa cha lori na bodi za mbao. Abiria hujazana ndani pamoja na mizigo yao, nao hubeba kila kitu, iwe ni majembe, au vyakula. Muziki unaofunguliwa kwa sauti ya juu na nyimbo zinazoimbwa kwa sauti ni mambo ya kawaida wakati wa safari. Vituo vya mabasi, ratiba, na barabara ambazo mabasi hayo hupitia hubadilika-badilika sana. “Basi la kwenda Vava‘u,” asema kiongozi mmoja wa safari, “halichelewi kamwe, saa zake za kufika ni wakati wowote ambapo litafika.”

      “Tulipotaka kununua kitu njiani,” asema John, “tulimwambia dereva asimamishe basi. Kisha baada ya kununua tulichotaka, tulipanda basi tena na kuendelea na safari yetu. Ajabu ni kwamba hakuna yeyote aliyejali.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki