Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • Mmoja wao alimhubiria binamu yake, Sauvao Toetu, aliyekuwa akiishi Faleasiu. Muda si muda, Sauvao na shemeji yake, Finau Feomaia, wakaanza kuhudhuria mikutano pamoja na familia zao na kuchukua msimamo upande wa kweli.

  • Samoa
    2009 Kitabu cha Mwaka cha Mashahidi wa Yehova
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 79]

      “Mtu wa Yehova”

      SAUVAO TOETU

      ALIZALIWA 1902

      ALIBATIZWA 1954

      MAELEZO MAFUPI KUMHUSU Mtu wa kwanza kukubali ukweli Faleasiu. Baadaye Jumba la Ufalme lilijengwa katika shamba lake. Limesimuliwa na mwana wake, Tafiga Sauvao

      MWAKA wa 1952, binamu ya baba yangu aliyekuwa akiishi Apia alitutembelea katika kijiji cha Faleasiu. Binamu huyo, aliyekuwa akishirikiana na Mashahidi wa Yehova, alitaka kuwa na mazungumzo ya Biblia pamoja baba yangu. Watu kadhaa wa ukoo wetu waliokuwa wakiishi katika kijiji hicho wakaamua kusikiliza. Walizungumza mfululizo kuanzia Jumamosi asubuhi mpaka Jumatatu (Siku ya 1) alasiri, na kwa muda wote huo walipumzika kwa kulala kwa saa moja tu. Baada ya mazungumzo kama hayo miisho-juma minne iliyofuata, baba yangu alisema hivi hatimaye: “Maswali yangu yote yamejibiwa. Nimeupata ukweli.” Hivyo basi, baba yangu, na shemeji yake, Finau Feomaia, pamoja na familia zao wakaikubali kweli.

      Baba yangu alianza kuhubiri mara moja. Hilo liliwashangaza watu wa ukoo, waliomwona kuwa mfuasi sugu wa dini ya Sabato. Walikuwa wakimdhihaki kwa kumwita mtu wa Yehova. Hata hivyo, ilikuwa sifa nzuri kama nini! Ingawa baba yangu hakuwa mtu mkubwa kimwili, alikuwa na moyo mkuu, naye alikuwa na akili nyingi na msemaji mwenye usadikisho. Hilo lilimwezesha kuitetea imani yake mpya kwa ustadi. Baada ya muda fulani kikundi chetu kidogo kikawa kutaniko la pili nchini Samoa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki