-
Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha KimbinguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na kiumbe hai wa kwanza ni kama simba, na kiumbe hai wa pili ni kama fahali mchanga, na kiumbe hai wa tatu ana uso kama wa mwanadamu, na kiumbe hai wa nne ni kama tai arukaye.” (Ufunuo 4:7, NW)
-
-
Uzuri Mwingi Mno wa Kiti cha Ufalme cha Yehova cha KimbinguUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Namna gani sasa yule kiumbe hai wa nne? Huyo anaonekana kama tai arukaye. Yehova mwenyewe anavuta fikira kwenye uwezo mkubwa wa kuona wa tai: “Mbali katika masafa marefu jicho lake hufuliza kutazama.” (Ayubu 39:29, NW) Kwa sababu hiyo, tai huyo anafananisha vizuri hekima yenye kuona mbali. Yehova ndiye Chanzo cha hekima. Makerubi wake hutumia hekima ya kimungu wanapotii amri zake.—Mithali 2:6; Yakobo 3:17.
-