Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ukweli Kuhusu Uchawi na Ulozi
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
    • 4. Watu wengi wanaamini nini kuhusu wachawi, nao wanatoa sababu gani ya kuamini hivyo?

      4 Katika sehemu nyingi za Afrika, watu wengi wanaamini kwamba binadamu anaweza kubadilika au kubadilishwa na kuwa mnyama. Wengi wanaamini kuwa wachawi wana uwezo wa kubadilika kuwa chui au nyoka. Hali kadhalika, watu wengi huhofu kwamba mchawi anaweza kuwabadili watu wengine kuwa wanyama. Katika Afrika magharibi, inaaminiwa kwamba wachawi wanaweza kutuma roho za wanadamu kupitia ndege au wanyama wengine ili kuwadhuru watu wengine. Waafrika wengi huhisi kwamba mabadiliko hayo ya mtu kuwa mnyama yamethibitishwa na watu fulani waliojionea kwa macho. Wao hudai kwamba zile hadithi nyingi zinazosimuliwa na watu wenye akili timamu haziwezi kuwa mambo ya kukisia tu.

  • Ukweli Kuhusu Uchawi na Ulozi
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
    • 10. Ni nini ambacho husemwa kuwahusu wachawi, na tunajuaje kwamba huo ni uwongo?

      10 Uwongo wa pili ambao Shetani huendeleza ni huu: Wachawi wanaweza kubadilika au kubadilishwa kuwa wanyama ili kuwadhuru wengine. Hebu jiulize: ‘Ikiwa wachawi wanaweza kufanya hivyo, ni nini hasa hutoka katika mwili na kuingia ndani ya mwili wa mnyama?’ Kama tulivyoona, roho si kitu kinachoweza kuuacha mwili wa mtu. Roho ni nguvu ya uhai ambayo huutia mwili nguvu lakini haiwezi kufanya chochote bila mwili. Kubadilika na kuwa mnyama ni kinyume cha sheria za maumbile zilizoanzishwa na Yehova Mungu. Bila shaka, Mungu hangepuuza sheria zake kwa kuwapa wanadamu uwezo wa kujibadili na kuwa wanyama wasio na akili.

      11. Tunajuaje kwamba wachawi hawawezi kuiacha miili yao au kujibadili kuwa wanyama, na je, wewe unaamini hilo?

      11 Roho haiwezi kuuacha mwili na kwenda kufanya jambo lolote baya au zuri. Hivyo, wachawi hawawezi kuiacha miili yao au kujibadili kuwa wanyama. Kwa kweli hawafanyi mambo wanayodai au wanayofikiri wamefanya.

      12. Ni kwa njia gani Shetani huwafanya watu waamini kwamba wamefanya mambo ambayo hawakufanya?

      12 Tunaweza kuelezaje mambo ambayo wale waliokuwa wachawi wanakiri kwamba walifanya? Shetani anaweza kufanya watu waamini kwamba wameona mambo ambayo hawakuona. Kupitia maono, Shetani anaweza kufanya watu wafikiri kwamba wameona, kusikia, au kufanya mambo ambayo hawakufanya. Kwa njia hiyo, Shetani anatarajia kugeuza watu wamwache Yehova na kuwafanya wafikiri kwamba Biblia si ya kweli.

  • Ukweli Kuhusu Uchawi na Ulozi
    Je, Umeipata Barabara Inayoongoza Kwenye Uhai wa Milele?
    • Je, Wachawi Wanaweza Kudhibiti Radi?

      Mapema mwaka wa 1977, wachawi 14 waliuawa kwa kuchomwa moto karibu na Pietersburg, Afrika Kusini. Gazeti la Drum la Afrika Kusini lilisema hivi kuhusu tukio hilo: “Wanaume na wanawake wameshikwa na woga. Wanaogopa kulogwa na kupigwa kwa radi  . . .

      “Ni lazima hatua fulani ichukuliwe . . . Kwa sababu hiyo, gazeti DRUM linawatolea wachawi wote mwito huu: Kuna pesa kiasi cha Randi 5 000 [sawa na dola 5,750 (za Marekani) wakati huo] kwenye ofisi zetu zitakazopewa yeyote ambaye katika mwezi wa Machi 1977, ataweza kumpiga na kumwua Stanley Motjuwadi kwa radi. Ikiwa hamwezi kufanya hivyo, basi acheni kila mtu ajue kwamba kule kujifanya kwamba mnaweza kudhibiti radi ni upumbavu na upuuzi mtupu.

      “Kwa hiyo, enyi wachawi waongo, anzeni kujitayarisha. Mpigeni na kumwua Stanley Motjuwadi kwa radi ikiwa mnaweza.”

      Je, wachawi hao waliweza kumpiga Stanley Motjuwadi kwa radi? Hapana, hawakuweza. Bw. Motjuwadi, mmoja wa waandishi wa Drum, hakufa bali alifanikiwa sana katika kazi yake na mwishowe akawa mhariri wa gazeti hilo.

      Sanduku: Mwandishi mmoja nchini Afrika Kusini aliwatolea wachawi mwito gani, na matokeo yakawaje?

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki