-
Ubaguzi Dhidi ya WanawakeAmkeni!—1998 | Aprili 8
-
-
Msimamizi wa Benki ya Dunia alieleza hivi: “Wanawake hufanya thuluthi mbili ya kazi za ulimwengu. . . . Lakini wao huchuma tu sehemu moja ya kumi ya mshahara wa ulimwengu na humiliki chini ya asilimia moja ya mali ya ulimwengu. Wako kati ya walio maskini zaidi wa maskini wa ulimwengu.”
-
-
Ubaguzi Dhidi ya WanawakeAmkeni!—1998 | Aprili 8
-
-
Akina Mama na Watoa-Riziki
Mzigo wenye kulemea wa kuitunza familia mara nyingi humwangukia zaidi mama. Yaelekea yeye hufanya kazi kwa muda wa saa nyingi na aweza pia kuwa ndiye mtoa-riziki pekee. Katika sehemu fulani za mashambani katika Afrika, karibu nusu ya familia zote husimamiwa na wanawake. Katika mahali fulani katika nchi za Magharibi, idadi kubwa ya familia husimamiwa na mwanamke.
Zaidi ya hilo, hasa katika nchi zinazositawi, kwa kawaida wanawake hufanya kazi zilizo ngumu zaidi, kama vile kuteka maji na kutafuta kuni. Ukataji wa misitu na kulisha wanyama kupita kiasi kumezifanya kazi hizi kuwa ngumu hata zaidi. Katika nchi fulani zinazoathiriwa na ukame, wanawake hutumia muda wa saa tatu au zaidi wakitafuta kuni na muda wa saa nne kila siku wakiteka maji. Wanapomaliza kufanya kazi hii ngumu, ndipo tu wawezapo kufanya kazi wanayotarajiwa kufanya nyumbani na shambani.
-