-
Twaa Fursa Hii ya Pekee!Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 15
-
-
PETER alikuwa ameendelea sana katika masomo yake ya kitiba, ujumbe wa Biblia wa wokovu uliponasa upendezi wake. Alipohitimu na kuanza kufanya kazi akiwa daktari katika hospitali, wakubwa wake waliendelea kumtia moyo afanye masomo maalumu ya kuwa mpasuaji wa nyuroni. Hapo palikuwa na fursa ambayo madaktari wapya wengi wangetwaa bila kusita.
Hata hivyo, Petera aliamua kutotwaa fursa hiyo. Kwa nini? Je, alikosa tu tamaa ya kufuatia makuu na msukumo unaohitajiwa? La, kwa kuwa Peter alifikiria toleo hilo kwa uangalifu. Baada ya kuwa Shahidi wa Yehova aliyejiweka wakfu na kubatizwa, alitamani kutumia wakati mwingi iwezekanavyo katika sehemu mbalimbali za huduma ya Kikristo. Yeye alisababu kwamba, mara angestahili kuwa mpasuaji wa nyuroni, kazi yake ingezidi kutumia wakati wake na nishati yake. Je, alikuwa mpumbavu kuacha taraja hilo lenye umashuhuri, au alikuwa mwenye hekima?
-
-
Twaa Fursa Hii ya Pekee!Mnara wa Mlinzi—1996 | Novemba 15
-
-
Peter—yule kijana aliyetajwa mwanzoni—alifikiria uamuzi wake kwa uangalifu akapima machaguo yake. Aling’amua kwamba lisingekuwa kosa kwake kufanya masomo kwa kusudi la kuwa mpasuaji wa nyuroni. Lakini ni nini kilichokuwa cha maana zaidi kwake? Ni utendaji wake katika huduma ya Kikristo, kwa kufikiria hali ya hima ya kazi hii. Wakati uo huo, alikuwa na wajibu mbalimbali wa kutimiza. Alikuwa ameoa na alihitaji kumtegemeza mkewe, aliyekuwa akishiriki katika kazi ya kuhubiri wakati wote. (1 Timotheo 5:8) Peter alihitaji pia kulipia madeni yaliyohusu elimu yake. Basi aliamua kufanya nini?
Peter aliamua kufanya masomo maalumu katika rediolojia na kufanya uchunguzi wa kikamili wa maradhi kwa kutumia kiuka sauti. Kazi hiyo ingehusisha siku ya kawaida ya kazi. Yeye angepata mazoezi yake pia katika saa za kawaida za kazi. Ndiyo, huenda watu fulani wakaona hilo kuwa wadhifa usio mashuhuri sana, lakini ungempa wakati zaidi wa kutolea ufuatiaji mbalimbali wa kiroho.
Jambo jingine la kufikiriwa lilichochea uamuzi wa Peter. Bila kuwahukumu wengine ambao huenda wakawa wameamua tofauti, alijua kwamba kuhusika sana katika mambo ya kilimwengu kwa kweli humtia Mkristo hatarini. Kwaweza kumfanya apuuze madaraka ya kiroho. Hilo latolewa kielezi na kielelezo kingine kilichohusisha kazi ya kuajiriwa.
-