Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • na, la kuduwaza zaidi, choo aina ya tube worm wenye minyiri-minyiri ya rangi nyekundu iliyoiva wanaojishikilia kwa nguvu kwenye sakafu ya bahari na kufikia kimo cha meta 1.8.

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Kiumbe Asiyeeleweka

      Wanabiolojia walipowachunguza tube worm, waligundua kwamba ni viumbe wasioeleweka. Hawakuwa na kinywa wala mfumo wa umeng’enyaji. Swali likazuka, Wao hulaje na kufyonza chakula chao? Kisha wakagundua jambo lenye kuduwaza: Choo hao walikuwa na damu nyekundu—si umajimaji tu bali damu halisi, yenye himoglobini nyingi—inayozunguka katika mwili wao na katika minyiri-minyiri yao inayoshabihi manyoya.

      Mafumbo hayo yalizidi kuwa tata wakati wanabiolojia walipopasua kifuko cha ute katika mwili wa tube worm. Tishu zake zilikuwa na mchanganyiko wa bakteria zipatazo bilioni 10 kwa kila gramu ya tishu! Mnamo mwaka wa 1980 mwanafunzi mmoja wa biolojia alibuni nadharia ya kwamba tube worm huishi kwa utegemeano—utegemeano huwawezesha viumbe wawili kupata manufaa kwa kushirikiana. Utafiti ulithibitisha nadharia yake kwa kuonyesha kwamba tube worm, akiwa kimelewa, hulisha bakteria hizo, na bakteria humlisha.

      Kama mashavu ya samaki, minyiri-minyiri ya tube worm hukusanya oksijeni na kaboni, vitu vinavyotumiwa na bakteria kutengenezea chakula. Minyiri-minyiri hiyo haipeperuki moja kwa moja kwenye maji moto yanayomiminwa na matundu—kufanya hivyo kungekuwa kuhatarisha uhai—bali hupeperuka katika sehemu ambako maji moto ya matundu huchanganyika na maji baridi sana ya baharini. Bila shaka, utengenezaji huo wa chakula huhitaji nishati. Katika uso wa dunia—na juu-juu ya bahari—nuru ya jua huandaa nishati muhimu kwa utengenezaji wa chakula kwa kusababisha ukuzi wa mimea. Lakini nuru ya jua haifiki hata kidogo katika lindi kuu anamoishi tube worm.

  • Sakafu ya Bahari—Siri Zake Zafunuliwa
    Amkeni!—2000 | Novemba 22
    • Ili kuweza kuchanganya kemikali zote zinazohitajiwa na bakteria, damu ya tube worm ina molekuli za himoglobini ambazo ni kubwa mara 30 zaidi ya molekuli za himoglobini katika mwili wa mwanadamu. Damu husafirisha kemikali hizo kwa bakteria zenye njaa, kisha bakteria humtengenezea tube worm chakula.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki