Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 20. (a) Ni katika maana gani watu huabudu hayawani-mwitu? (b) Ni kwa nini Wakristo ambao huabudu Yehova Mungu hawashiriki ibada hiyo ya hayawani-mwitu, nao wanafuata kielelezo cha nani?

      20 Ibada katika maana gani? Katika maana ya kuweka upendo wa nchi mbele ya upendo wa Mungu. Watu walio wengi wanapenda bara la uzawa wao. Wakiwa wananchi wema, Wakristo wa kweli wanaheshimu pia watawala na mifano ya nchi ambako wao wanakaa, wanatii sheria, na kuchangia kihakika masilahi ya jumuiya yao na majirani wao. (Warumi 13:1-7; 1 Petro 2:13-17) Hata hivyo, wao hawawezi kujitoa kipumbavu kwa ajili ya nchi moja dhidi ya zile nyingine zote. “Nchi yetu, ikosee isikosee” si fundisho la Kikristo. Kwa hiyo Wakristo wanaomwabudu Yehova Mungu hawawezi kushiriki kutoa ibada ya kizalendo yenye kiburi kwa sehemu yoyote ya hayawani-mwitu, kwa kuwa hiyo ingekuwa ni kuabudu drakoni—chimbuko la mamlaka ya huyo hayawani. Wao hawawezi kuuliza kwa kusifu mno: “Ni nani aliye kama hayawani-mwitu?” Badala ya hivyo, wao wanafuata kielelezo cha Mikaeli—jina lake likimaanisha “Ni Nani Aliye Kama Mungu?”—wanapotegemeza enzi kuu ya ulimwengu wote mzima ya Yehova.

  • Kupambana na Hayawani Wawili Wakali Sana
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Hivyo, kufikia mwishoni mwa 1914 kuendelea mpaka ndani ya 1918, wakati mataifa yenye kupigana yalipokuwa yakiraruana kihalisi kama hayawani-mwitu, wananchi wa mataifa hayo walibanwa wamwabudu hayawani-mwitu, washiriki dini ya utukuzo wa taifa, hata kuwa tayari kufia nchi yao.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki