-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
naye mfalme wa nne atakuwa tajiri kuliko hao wote; naye atakapopata nguvu kwa utajiri wake, atawachochea wote juu ya ufalme wa Uyunani [“Ugiriki,” NW].” (Danieli 11:2)
-
-
Wafalme Wawili WapambanaSikiliza Unabii wa Danieli!
-
-
Alimwachia mwana wake Shasta wa Kwanza, ambaye alitawala pia baada yake akiwa mfalme “wa nne.” Ndiye Mfalme Ahasuero aliyemwoa Esta.—Esta 1:1; 2:15-17.
6, 7. (a) Mfalme wa nne ‘aliwachocheaje wote juu ya ufalme wa Ugiriki’? (b) Vita ya Shasta dhidi ya Ugiriki ilikuwa na matokeo gani?
6 Shasta wa Kwanza kwa kweli ‘aliwachochea wote juu ya ufalme wa Ugiriki,’ yaani, yale majimbo huru ya Ugiriki yote pamoja. “Akihimizwa na maofisa wa serikali yake wenye kutaka makuu,” chasema kitabu The Medes and Persians—Conquerors and Diplomats, “Shasta alishambulia toka nchi kavu na baharini.” Mwanahistoria Mgiriki Herodotus, wa karne ya tano K.W.K., aandika kwamba “hakuna mashambulizi mengine yaliyolingana na hili.” Rekodi yake yataarifu kwamba jeshi la majini “lilijumlika kuwa watu 517,610. Askari-jeshi walikuwa 1,700,000; wapanda-farasi walikuwa 80,000; na kuongezea Waarabu waliopanda ngamia, na Walibya waliopigana wakiwa kwenye magari ya vita, ninaokadiria walikuwa 20,000. Kwa hiyo, wanajeshi wote wa nchi kavu na wa majini walijumlika kuwa watu 2,317,610.”
7 Akipanga kupata ushindi kamili, Shasta wa Kwanza aliliongoza jeshi lake kubwa likapigane na Ugiriki mwaka wa 480 K.W.K. Waajemi waliharibu kabisa Athene waliposhinda mbinu ya Ugiriki ya kukawia huko Thermopylae. Hata hivyo, walipofika Salamis walishindwa vibaya. Ugiriki ilishinda tena huko Plataea, mwaka wa 479 K.W.K.
-