-
Kuuchunguza Mwili Bila Kufanya UpasuajiAmkeni!—2008 | Novemba
-
-
Sonography
Inafanyaje kazi? Kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti au sonography ni tekinolojia ya kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti yasiyoweza kusikiwa na wanadamu. Mawimbi yanapofika mahali kuna badiliko katika tishu, kwa mfano, mahali kuna kiungo, mawimbi huongezeka. Kompyuta hupima mawimbi na kuonyesha muundo wa kiungo, kama vile kina, ukubwa, na umbo lake. Mawimbi yenye sauti za chini husaidia kuchunguza sehemu za ndani kabisa za mwili; mawimbi yenye sauti za juu sana husaidia kuchunguza sehemu za juu za viungo kama vile macho na ngozi, labda hata kusaidia kutambua kansa ya ngozi.
Katika visa vingi, mtaalamu hutumia kifaa kinachoitwa transducer. Anapopaka mafuta juu ya ngozi, anasugua kifaa hicho juu ya eneo linalochunguzwa, na picha hutokea mara moja kwenye kompyuta. Inapohitajika transducer ndogo inaweza kuunganishwa na kifaa fulani na kuingizwa mwilini ili kuchunguza sehemu fulani za mwili.
Tekinolojia inayoitwa Doppler ultrasound hutambua kitu kinachosonga na inatumiwa kuchunguza jinsi damu inavyosonga. Hilo linaweza kusaidia kutambua magonjwa yanayohusiana na viungo na uvimbe ambao kwa kawaida huwa na mishipa mingi sana ya damu.
Mbinu hii ya kutumia mawimbi ya sauti husaidia madaktari kutambua magonjwa mbalimbali na kisababishi cha matatizo mbalimbali kama vile, magonjwa ya moyo, uvimbe katika matiti, au afya ya mtoto tumboni. Kwa upande mwingine, kwa kuwa mawimbi ya sauti hayawezi kupenya gesi, mbinu hiyo haifanyi kazi vizuri inapotumiwa katika sehemu fulani za tumbo. Pia, huenda picha isiwe wazi kama ile inayotolewa kupitia njia nyingine.
Madhara: Kwa kawaida mawimbi ya sauti yanapotumiwa vizuri hayana madhara, hata hivyo, yanaweza kudhuru tishu kutia ndani zile za kijusi. Kwa hiyo, huenda mawimbi ya sauti yakamdhuru mama mjamzito.
Faida: Tekinolojia hii inatumiwa katika sehemu nyingi, si lazima mgonjwa afanyiwe upasuaji, na ni mbinu isiyogharimu sana. Pia, picha hutokezwa mara moja.
-
-
Kuuchunguza Mwili Bila Kufanya UpasuajiAmkeni!—2008 | Novemba
-
-
[Picha katika ukurasa wa 14]
Sonography
-