Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ninaweza Kupata Wapi Burudani Inayofaa?
    Amkeni!—2011 | Novemba
    • MUZIKI

      Weka alama ya ✔ kando ya aina ya muziki upendao zaidi.

      ○ Roki

      ○ Muziki wa zamani

      ○ Jazi

      ○ R&B

      ○ Rapu

      ○ Nyingine

      Je, wajua . . . ? Kampuni nne kubwa za kurekodi hutoa jumla ya vibao 30,000 hivi kila mwaka.

      Mambo ya kuepuka. Kama tu ilivyo na sinema na vitabu, aina nyingi za muziki wa leo huwa na mambo machafu. Maneno machafu na video za muziki zenye picha chafu zinaweza kufanya iwe vigumu kudhibiti tamaa yako ya ngono. (1 Wakorintho 6:18) Leigh, mwenye umri wa miaka 21 anasema kwamba “muziki mwingi leo huwachochea watu wajiendeshe kwa njia inayopingana na viwango vya Biblia, na mdundo wake huwachochea wacheze dansi kwa njia inayoamsha hamu ya ngono.”

      Jinsi unavyoweza kuchagua. “Mimi hujiuliza, ‘Ikiwa ningewaruhusu Wakristo waliokomaa wachunguze orodha yangu ya muziki, je, ningeaibika wanapoona muziki ninaosikiliza?’ Hilo hunisaidia nichague kwa hekima muziki nitakaosikiliza.”—Leanne.

      Dokezo. Uwe tayari kusikiliza mitindo mbalimbali ya muziki. “Baba yangu hufurahia kusikiliza muziki ya zamani, kwa hiyo nilisikiliza muziki wa aina hiyo tangu nilipokuwa mchanga,” anasema kijana anayeitwa Roberto. “Akili yangu ilipanuka nilipojifunza kuhusu muziki wa zamani huku nikijifunza pia kupiga piano!”

      Jiulize hivi,

      ‘Je, muziki ninaosikiliza unafanya iwe rahisi—au vigumu—kwangu kudhibiti tamaa ya ngono?’

  • Ninaweza Kupata Wapi Burudani Inayofaa?
    Amkeni!—2011 | Novemba
    • [Sanduku/​Picha katika ukurasa wa 19]

      “Muziki fulani unaweza kutufanya tuvutiwe na mambo ambayo tukiwa Wakristo tunapaswa kujiepusha nayo. Hatungependa kupuuza maonyo ya dhamiri yetu nzuri kwa sababu tu tunapenda mdundo fulani.” Janiece

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki