Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Ngono Itafanya Urafiki Wetu Uwe Mzuri Zaidi?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
    • Ukipuuza sheria za asili, kama vile sheria ya uvutano, utapatwa na madhara. Ndivyo ilivyo pia ukipuuza sheria za maadili, kama ile inayosema: “Mjiepushe na uasherati.” (1 Wathesalonike 4:3) Kutotii amri hiyo kuna madhara gani? Biblia inasema: “Aliye na mazoea ya kufanya uasherati anautendea dhambi mwili wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 6:18) Kwa njia gani? Jaribu kuorodhesha madhara matatu yanayoweza kuwapata wale wanaofanya ngono kabla ya ndoa.

      1 ․․․․․

      2 ․․․․․

      3 ․․․․․

      Sasa tazama mambo uliyoandika. Ulitia ndani mambo kama vile ugonjwa wa zinaa, mimba haramu, au kupoteza kibali cha Mungu? Bila shaka, hayo ni matokeo mabaya yanayoweza kumpata mtu yeyote anayepuuza sheria ya Mungu ya maadili kuhusu uasherati.

  • Je, Ngono Itafanya Urafiki Wetu Uwe Mzuri Zaidi?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
    • Wachunguzi wamegundua kwamba vijana wengi kati ya hao hupata angalau moja kati ya mambo yafuatayo yenye kushangaza.

      MSHANGAO WA 1 DHIKI. Vijana wengi ambao wamefanya ngono kabla ya ndoa wanasema kwamba walijuta baadaye.

      MSHANGAO WA 2 KUTOAMINIANA. Baada ya kufanya ngono kila mmoja huanza kujiuliza, ‘Amefanya ngono na nani mwingine?’

      MSHANGAO WA 3 KUCHANGANYIKIWA KIMAWAZO. Tamaa ya moyoni ya wasichana wengi ni kuwa na mtu atakayewalinda, si kuwatumia. Nao wavulana wengi hawavutiwi tena na msichana baada ya kufanya ngono naye.

      Pamoja na hayo, wavulana wengi husema kwamba hawawezi kumwoa msichana ambaye wamefanya ngono naye. Kwa nini? Kwa sababu wangependa mtu aliye safi!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki