Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Tukio Lenye Kufurahisha Katika Nchi za Balkan
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 15
    • Tukio Lenye Kufurahisha Katika Nchi za Balkan

      Mnamo mwaka wa 1922, Wanafunzi wa Biblia Wenye Bidii, kama Mashahidi wa Yehova walivyoitwa wakati huo, walifanya mkutano huko Innsbruck, Austria. Kijana mmoja aliyeitwa Franz Brand, kutoka mji wa Apatin, Vojvodina, huko Serbia, alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mkutano huo. Mara tu msemaji alipotaja jina la Mungu, Yehova, kikundi fulani cha watu kilianza kumzomea, akashindwa kuendelea, hivyo mkutano huo ukavunjwa. Lakini Franz aliguswa moyo sana na habari hiyo, akaanza kuhubiri habari njema za Ufalme. Huo ulikuwa mwanzo mdogo wa ukuzi wa kiroho wenye kusisimua katika mojawapo ya nchi za Balkan.

  • Tukio Lenye Kufurahisha Katika Nchi za Balkan
    Mnara wa Mlinzi—2002 | Oktoba 15
    • Ukuzi wa Kiroho Katika Nchi za Balkan

      Franz Brand alisisimuliwa sana na kweli mpya alizosikia, akaazimia kueneza habari njema. Aliajiriwa kazi ya kinyozi katika mji wa Maribor, nchini Slovenia karibu na mpaka wa Austria. Alianza kuwahubiria wateja wake ambao kwa kawaida waliketi kwa utulivu na kumsikiliza huku wakinyolewa. Kwa sababu ya jitihada zake, kikundi kidogo cha wahubiri wa Ufalme kilianzishwa katika mji wa Maribor mwishoni mwa miaka ya 1920. Hotuba zinazotegemea Biblia zilitolewa katika mkahawa mmoja ambao uliitwa jina lifaalo, Mkahawa wa Novi svet (Ulimwengu Mpya) Unaopika Chakula Kinachotoka Baharini.

      Baada ya muda, habari njema zilihubiriwa katika nchi yote. Kutumiwa kwa “Photo-Drama of Creation” (onyesho la saa nane la filamu, slaidi, na rekodi) kulisaidia sana ukuzi huo. Mapainia Wajerumani waliotorokea Yugoslavia wakati Mashahidi wa Yehova walipokuwa wakiteswa vikali nchini Ujerumani katika miaka ya 1930, waliwatia nguvu Mashahidi nchini Yugoslavia. Walijitoa kabisa kuhubiri maeneo yaliyo mbali sana katika nchi hiyo yenye milima-milima bila kujali mapendezi yao ya kibinafsi. Mwanzoni, watu wengi hawakukubali ujumbe wao. Mapema miaka ya 1940, ni wahubiri 150 tu waliotoa ripoti ya utumishi wa shambani.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki