Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 3/8 uku. 32
  • “Yamekuwa Yenye Kupendeza Sana!”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Yamekuwa Yenye Kupendeza Sana!”
  • Amkeni!—1996
Amkeni!—1996
g96 3/8 uku. 32

“Yamekuwa Yenye Kupendeza Sana!”

“Sikuzote mimi nimefurahia kusoma Mnara wa Mlinzi na Amkeni!, lakini yamekuwa yenye kupendeza sana katika miaka ya majuzi hivi kwamba ni vigumu kupata maneno ya kuyaeleza. Nataka kuonyesha uthamini wangu kwa ajili ya habari iliyotolewa kwenye matoleo ya Amkeni! ya Oktoba 22 na Novemba 8, 1994 chini ya vichwa “Wakati Dini Ijiungapo na Vita” na “Sarajevo—Kutoka 1914 Hadi 1994.” Ile vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Bosnia-Serbia-Kroatia ni hali inayotatanisha na yenye kuleta msiba lakini igusayo moyo sana nikiwa Mkroatia. Nilipendezwa hasa na jinsi mlivyofuatia historia ya vita hiyo hadi kwenye vyanzo vyayo huko nyuma kwenye mwaka 1054. Hilo lilionyesha wazi fungu la dini na juhudi zayo zisizokoma ambazo zimeongoza kwenye migawanyiko zaidi na chuki kati ya vikundi vya kitaifa. Kwa kuhuzunisha, ulimwengu leo unaweza kuona yaliyo mabaya tu katika watu hawa ambao kwa asili ni watu wazuri. Asanteni tena kwa kufanya hali isiyoweza kufahamika ieleweke. M. K.”

Amkeni! limeimarisha sifa ya kufanya utafiti kwa uangalifu na kutoa ripoti za uhakika. Hilo pia ni gazeti linalotoa tumaini la wakati ujao wenye amani lenye msingi katika ahadi ya Mungu ya kuifanya dunia iwe chini ya utawala wa Ufalme wake.

Ikiwa ungependa kusoma gazeti hili kwa ukawaida, wasiliana na Mashahidi wa Yehova katika eneo lako, au uandike kwenye anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa wa 5 wa toleo hili.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 32]

Kulia: Picha za Culver

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki